Kwenye playlist ya Radio za Tanzania sasa
hivi kunayo single ya Sophia pia ambayo original yake imefanywa na Ben
Pol lakini Peter Msechu kaifanyia kazi na kuitoa remix yake.
Kama ulikua hujui, haya ndio maneno ya Ben Pol baada ya Peter Msechu kuirudia >>> ‘Kiukweli
mimi nimependa sana na alinitumia, unajua hivi vitu ni lazima mtu
anakushirikisha sababu wewe umetunga, una producer wako, manager
wako…….. nimependa sana kuliko labda nyimbo ingetoka unakutana nayo‘
‘Msechu
alinipigia simu akaniambia, niliona hii ni heshima kubwa sana na Msechu
ni miongoni mwa ninaowakubali, nimeisikiliza single nimedata, Mswaki
Producer wangu pia nae kadata, tunaisikiliza kila saa…. ni kazi flani
nzuri sana, mpaka leo Mswaki ametoa wazo kwamba au tutoe beat chorus kwa
mtu anaetaka kufanya? mbona kama imekua inavutia?‘ – Ben Pol
Maneno ya Ben Pol unaweza kuyasikiliza hapa chini pia pamoja na hiyo single aliyorudia Msechu.
Maneno ya Ben Pol unaweza kuyasikiliza hapa chini pia pamoja na hiyo single aliyorudia Msechu.


Post a Comment