Niwiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiwa na
imani kwamba Mungu amekujaalia uzima na unaendelea vyema na majukumu
yako ya kila siku kama kawaida.Mimi kama ilivyo ada yangu, namshukuru
Mungu kwa kila jambo ambalo amekuwa akinitendea katika maisha yangu ya
kila siku.
Kikubwa nimshukuru kwa kunipa uwezo wa kuandika mambo ambayo yamekuwa
ni yenye msaada kwa wengi walio kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Niseme tu kwamba, maisha yetu bila mapenzi hayajakamilika. Hata uwe
mgumu vipi lakini kuna wakati utahitaji mwenza ambaye atayakamilisha
maisha yako.Ndiyo maana kila mmoja ana haki ya kupenda. Hakuna anayeweza
kukushangaa kukuona umetokea kumpenda fulani kwa kuwa ni jambo
linalokuja ‘automatikale’. Ukipenda umependa, huwezi kujizuia.
Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, leo nataka kuzungumzia jambo ambalo
limekuwa likiwaweka wengi kwenye wakati mgumu. Ni kweli kabisa una haki
ya kupenda lakini wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa,
hutakiwi kupenda kupita kiasi.
Wazungu wanasema ‘too much is harmful’, wakimaanisha kwamba katika
kila jambo ukizidisha kipimo ni hatari. Kumpenda mtu sana nako ni tatizo
na ndiyo maana umekuwepo ‘ugonjwa’ unaoitwa KKK, yaani Kupenda Kupita
Kiasi.
Ukijaribu kufanya uchunguzi utabaini wapo watu ambao wanawapenda wapenzi wao mpaka wamechanganyikiwa.
Hawa ni wale wanaofikia hatua ya kusema; ‘bila fulani siwezi kuishi’.
Eti kwa sababu amempenda flani basi ikitokea ameachwa ni bora afe
kuliko kuendelea kuishi, hii ni mbaya sana!
Ni mbaya kwa sababu wapo watu kweli waliofikia hatua ya kunywa sumu, kuchanganyikiwa na hata kushindwa kufanya shughuli zao kwa ufasaha kwa kuwa wametoswa na watu wanaowapenda. Haya ni mapenzi au uchizi?
Ni mbaya kwa sababu wapo watu kweli waliofikia hatua ya kunywa sumu, kuchanganyikiwa na hata kushindwa kufanya shughuli zao kwa ufasaha kwa kuwa wametoswa na watu wanaowapenda. Haya ni mapenzi au uchizi?
Wakati
mwingine hali inakuwa mbaya zaidi pale ambapo unamkuta mwanaume
anampenda sana msichana flani wakati ameshaambiwa kuwa hapendwi. Licha
ya kupewa jibu hilo bado anang’ang’ania kwa sababu tu amependa
kupitiliza, hii siyo sawa hata kidogo.
Penda kwa kiasi, onyesha hisia zako kwa mtu ambaye unaamini
atayafanya maisha yako yawe ni yenye furaha lakini ukiona unayempenda
hana chembe za kukupenda, chukulia ni sawa kisha uyaache maisha yako
yaendelee.
Hata kwa walio kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida wanatakiwa kujizuia
kupenda kupita kiasi na wala hawatakiwi kuonyesha kwamba ‘wamekufa na
wameoza’. Kufanya hivyo ni kuingiza mizizi kwenye uhusiano ambao huna
uhakika wa kudumu.
Ni wangapi unaowajua ambao walipenda kupita kiasi lakini leo hii
wananyanyasika kama siyo kuachwa kabisa? Wapo wengi sana huko
mtaani.Kimsingi kwa maisha ya sasa yalivyo, tunatakiwa kuwa makini sana
katika kupenda kwa kuzingatia yafutayo;
Kwanza, mpende yule anayeonesha kukupenda na hakikisha unamfanya
aamini kwamba unampenda kutoka moyoni mwako.Pili, usikubali akutesa kisa
umempenda. Ukiona analipiga teke penzi lako, chukulia kwamba umependa
pasipo na penzi hivyo achana naye.
Tatu, hata kama unahisi kumpenda sanaaa, yeye ajue tu unampenda
lakini si kuonesha kwa kiwango gani.Nne, zungumza na moyo wako na
‘uukontroo’ usipende sana. Madhara ya kupenda sana yanajulikana ikiwa ni
pamoja na kujitafutia vidonda vya tumbo, upo?
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo

Post a Comment