Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (mbele ) akiongoza kikao
kilichokutanisha ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya
Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini
inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya
kuboresha miradi hiyo.
……………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameliomba Shirika la Fedha
Duniani (WB) kulisaidia Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) ili liweze
kuimarisha miradi ya usambazaji wa umeme nchini hususan vijijini.
Simbachawene aliyasema hayo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya kuboresha miradi hiyo.

Alisema
kuwa Tanesco inakabiliwa na changamoto ya fedha katika utekelezaji wa
miradi ya umeme hususan usambazaji wa umeme vijijini na kupelekea miradi
mingi kutokamilika kwa wakati.
Akielezea
maendeleo ya shirika hilo la umeme, Simbachawene alisema kuwa shirika
hilo limeongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato kwa kubuni mikakati
mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato hayo na kupunguza hasara zilizokuwa
zikijitokeza mara kwa mara.
Akielezea
kuhusu upunguzaji wa bei ya umeme nchini, Simbachawene alisema kuwa
Serikali imejenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es
Salaam jambo litakalochangia upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika
na kwa gharama nafuu ambalo ni moja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa.
“
Ili kuhakikisha wananchi wananufaika na sekta mpya ya gesi, serikali
ilibuni utaratibu wa kusomesha wataalam pamoja na wanafunzi waliofanya
vizuri katika masomo ya sayansi katika vyuo vikuu vinavyotoa fani za
mafuta na gesi ili kuwa na wataalamu watakaosimamia kwa ufanisi sekta ya
gesi na mafuta.,” alisema Simbachawene .
Aliongeza
kuwa mara baada ya kuwa na wataalam waliobobea katika masuala ya gesi
na mafuta, serikali itaunda taasisi itakayokuwa na kazi ya kutoa ushauri
katika masuala ya gesi na mafuta hususan wakati wa uingiaji wa
mikataba.
“ Kwa mfano kuna uwekezaji mkubwa unaohitaji mamilioni ya Dola za Marekani, kwa mfano Ujenzi wa Viwanda vya Gesi ya Kimiminika (LNG), uwekezaji huu unahitaji timu ya wataalam watakaohakikisha kuwa maslahi ya nchi yanazingatiwa,” alisisitiza Simbachawene.
Aliongeza
kuwa, mbali na kuzalisha wataalam, serikali kwa sasa inaandaa sheria
kwa ajili ya sekta za gesi na mafuta ambapo mpaka sasa maoni kutoka kwa
wadau mbalimbali yamekusanywa na kujumishwa.
Akielezea kuhusu uwazi katika mikataba ya gesi na mafuta, Simbachawene alisema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kunakuwepo na uwazi katika shughuli zake, moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kujiunga na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) ambapo taarifa mbalimbali za malipo na makusanyo katika sekta za madini na gesi zimekuwa zikikusanywa na kusambazwa kwa wananchi.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inafuata sheria zinazosimamia utoaji wa taarifa za mikataba.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier alisema kuwa Benki ya Dunia ipo tayari kushirikiana na Serikali kupitia Shirika la Tanesco ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika na nchi kutoka katika kundi la nchi masikini dunaiani na kuwa katika kundi la nchi zenye kipato cha kati.

Dongier
alisema awali Benki ya Dunia ilijitosa kuisaidia Tanesco ili iweze
kutoka kwenye utegemezi wa chanzo kimoja cha nishati ya umeme yaani maji
na kutumia vyanzo vingi ikiwa ni pamoja na kupelekea ujenzi wa bomba la
gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es salaam ambalo mara baada ya
ukamilishwaji wake litapunguza gharama ya uzalishaji wa umeme na
wananchi wengi kunufaika na nishati hiyo.
Pia
Dongier alimpongeza Waziri Simbachawene kwa hatua ya serikali kujenga
bomba la gesi na kasi ya uandaaji wa sera kwa ajili ya usimamizi wa
sekta mpya za gesi na mafuta na kusisitiza kuwa Benki ya Dunia ipo
tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa malengo yake
yanatekelezwa.
Post a Comment