TAARIFA YA NYONGEZA/UFAFANUZI YA TUKIO LA KULA
NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AKIWA HOSPITALI
Leo tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu cha
Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe 29/03/2015. Silaha
hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia
zilikamatwa risasi 17 za Short Gun.
Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:
Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba silaha hiyo
inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat
Gwajima. Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima anamiliki
Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837 ambayo inatumia risasi za aina ya
hizo zilizokamatwa.
Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu
kumtorosha Askofu Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea.
Aidha watu hao
pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi zilizotajwa hapo juu
wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo na risasi hizo na idadi iliyotajwa
kwa mujibu wa sheria.
Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa
mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili sheria ichukue
mkondo wake.
Post a Comment