HAJAKOMA? Staa wa Bongo Fleva anayesumbua na wimbo
wa Chumvini, Khaleed Mohamed ‘TID’ amehusishwa na msala mwingine baada
ya kudaiwa ku kumjeruhi James Richard, mkazi wa Jiji la Dar.
Endapo itathibitika kama ni kweli ametenda kosa hilo, TID atakuwa
yupo katika hatari ya kuswekwa gerezani kwa mara ya pili kwani mwaka
2008 alitiwa hatiani kwa kosa la kumpiga Ben Mashibe, mkazi wa jijini
Dar ambapo alifungwa jela mwaka mmoja kabla ya kuachiwa kwa msamaha wa
rais.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia tukio hilo, TID anadaiwa kutenda
kosa hilo maeneo ya Kinondoni-Sterio karibu na eneo analoishi ambalo
amelipachika jina la Unyamani.Akizungumza kwa masikitiko, James alisema
siku ya tukio, alifika maeneo hayo kukutana na rafiki yake, ghafla
alitokea TID na kuanza kumsema vibaya kisha kumrushia makonde kwa madai
kuwa aliegesha gari lake katika anga zake.
“Nilikuwa namsubiri mwenyeji wangu, ghafla alifika TID akiwa katika
gari lake ambapo alikaa humo ndani ya gari kama dakika 30 na alivyoshuka
alinisemea mbovu kisha kunivamia na kuanza kunipiga.
“Nikaishika cheni yake, akaivua na kuniachia kisha akaondoka. Baada ya muda alirudi akiwa amefuatana na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Abdallah au Dulla Manga wakiwa wameshika visu.
“Nikaishika cheni yake, akaivua na kuniachia kisha akaondoka. Baada ya muda alirudi akiwa amefuatana na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Abdallah au Dulla Manga wakiwa wameshika visu.
“TID akasema wewe ndiyo mwizi wangu wa cheni nipe cheni yangu haraka
sana kabla sijakutoa nyama za makalio, alinivamia na kuanza
kunishambulia kwa visu huku kaka yake akinishika ili kutoa nafasi kwa
mdogo wake kunishambulia atakavyo,” alisema James.
Khaleed Mohamed ‘TID’.
Alisema wakati anashambuliwa na TID, Dulla aliwaambia watu
waliokuwepo kuwa wasiamulie na ambaye angekaidi angemchoma kisu cha
chembe ambapo waliogopa mpaka alipofika mjumbe wa mtaani huo, akaamulia.
Alisema kuwa TID alimpiga kiasi ambacho uso ulivimba, kuteguliwa
mkono na kuchomwa visu kichwani na kisogoni ambako alitokwa damu nyingi
hadi wasamaria wema walipoungana na mjumbe kumsaidia kisha kumkimbiza
Kituo cha Polisi cha Oysterbay damu zikiwa zinamtoka chapachapa ambako
alipata hati ya polisi ya matibabu (PF3) na kufungua kesi iliyosomeka
OB/RB/3211/2013.
Kitendo hicho kiliwakasirisha polisi waliokuwa zamu ambapo mmoja wao
alisema anamshangaa TID kurudia kosa lililompeleka gerezani huko
nyuma.James alisema baada ya kufungua kesi hiyo, alikimbizwa katika
Hospitali ya CCBRT ambako alishonwa nyuzi nne katika jeraha la kisogoni
na kupatiwa dawa kwa ajili ya maumivu ya mkono na usoni ambako alivimba
sana.
“Leo naenda (Jumanne) naenda tena hospitali ili nijaziwe PF3 yangu
kwa ajili ya kulipeleka shauri hili mahakamani,” alisema James kwa
masikitiko.Jitihada za kumpata TID anayesakwa na jeshi la polisi ili
kusikia kauli yake kuhusiana na madai hayo hazikuzaa matunda kufuatia
simu yake kutopatikana hewani.
Hata hivyo, waandishi wetu wanaendelea kumtafuta.
Hata hivyo, waandishi wetu wanaendelea kumtafuta.
Post a Comment