Rais wa TWAA, Irene Kiwia akiongea jambo mara baaada ya kutangaza washindi.
..Mama Debora Mwenda atwaa tuzo ya ‘Lifetime Achievement Award’
Na Andrew Chale wa modewjiblog
Taasisi
ya Shirika la kijamii Tanzania Women of Achievement Awards (TWAA),
wamewatunukia tuzo Wanawake mbali mbali Nchini kwa mafanikio yao katika
tuzo za Wanawake wenye MafanikioTanzania zilizofanyika leo Machi 7,
katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, ambazo mwaka huu
zinafanyika kwa mwaka wa Saba, mfululizo tangu kuanzishwa kwake, likiwa
na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia
maendeleo Tanzania katika nyanja tofauti.
Katika
tuzo, Rais wa TWAA, Irene Kiwia aliweza kumtangaza Mwanamke
aliefanya vizuri ndani ya Mwaka mzima‘Woman of the Year’, ambapo tuzo
hiyo ilienda kwa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia,
Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba.
Mbali
na tuzo hiyo, kwa upande wa tuzo ya mwanamke aliefanya vizuri katika
maisha yake ‘Lifetime Achievement Award’, ilienda kwa Mama Debora
Mwenda ambaye kitaaluma alikuwa mwandishi wa habari na mcheza michezo ya
kuigiza miaka ya zamani, kupitia Redio Tanzania, (RTD), wakati huo.
Rais
wa shirika la Wanawake Wenye Mafanikio (TWAA), Irene Kiwia (kulia)
akimkabidhi tuzo ya Mwanamke wa Mwaka Mwenye mafanikio, Mkaguzi Msaidizi
wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia, Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca
Komba akipokea tuzo hiyo, iliyotolewa Machi 7, katika Hoteli ya
Serena, Jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake, Rais TWAA, Bi. Irene Kiwia alipongeza wadau mbalimbali
waliojitokeza kusaidia tuzo hizo. “Lengo la TWAA ni kusheherekea
mafanikio ya wanawake hawa na kazi wanazozifanya kwenye jamii kupitia
nyanja tofauti ndani ya Tanzania. Washindi waliopatikana ni kuzingatia
vigezo mbalimbali vilitumika katika kuwachagua kama vile utofauti
waliouonyesha katika jamii zao, jinsi gani wameweza kuwavutia na
kuwashawahi watu wengine, na jinsi gani wameweza kuwagusa na kuwafikia
watu tofauti tofauti.” Alieleza.
Aidha,
alimwelezea, Inspekta Prisca Komba kuwa ni mwanamama wa kuigwa kwani
ameweza kufanikisha uwepo wa dawati la Jinsia na namna
anavyowashughulikia masuala ya wanawake katika vituo vya Polisi, kesi
zinazowahusu, ambapo hali hiyo awali haikuwapo hapa Nchini kutokana na
jamii nyingi hasa jeshi la Polisi ikiwemo kwa wanawake wengi kukosa
fursa na haki zao za msingi hasa katika madawati ya mashitaka ya jeshi
la Polisi.
Bi.
Kiwia alisema kwamba “ Tuzo hizo zitakuwa zinaenda sambamba na na
mafunzo ya kujenga uwezo wa wasichana viongozi katika nyanja tofauti
walio kati ya umri wa miaka 18-27 kutoka mikoa yote ya Tanzania ambayo
yatachukua wiki 6.
Mama
Debora Mwenda (kushoto) akikabidhiwa tuzo maalum ya ‘Lifetime
Achievement Award’ kutoka kwa Dk. Darleana McHenry ambaye ni Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya St.Carrie’s Center inayojishughulisha na masuala ya
Elimu Duniani kote, tuzo hizo zimefanyika Machi 7, katika Hoteli ya
Serena, jijini Dar es Salaam.
Wasichana
hao watakutanishwa na wanawake wanaofanya vizuri katika biashara, kazi
za jamii na idara tofauti kwa ajili ya kupewa motisha na kujifunza.
Huku mategemeo yakiwa ni kuwa baada ya mafunzo hayo wasichana wataenda
kuwa chachu ya mabadiliko mikoani kwao na kuwafundisha wenzao wengi ili
kusambaza mori wa maendeleo na mabadiliko kwa wasichana wadogo nchini
kote.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa TWAA, Bi. Sadaka Gandhi alisema “suala la
uwezeshaji kwa wanawake linapewa kipaumbele duniani kote, tuzo hizi
zitaonyesha uwezo na ugunduzi wa wanawake katika sehemu tofauti.
Tunaamini kuwa wale wote walioshinda leo watakuwa chachu ya mabadiliko
kwa wasichana kutoka vijijijini, wafanyabiashara na wanawake wengi chini
Tanzania”.alisema Bi. Gandi.
Aidha,
tuzo zingine walizochukua wanawake hao ni pamoja na Sanaa na utamaduni,
ujasiriamali, elimu, afya, sayansi na teknolojia, kilimo, ustawi wa
jamii, michezo, umma, mshiriki wa mafanikio mwenye umri mdogo, mwanamke
aliefanya vizuri ndani ya mwaka mzima na mwanamke aliefanya vizuri
katika maisha yake.
Blandina Sembu wa kipindi cha Wanawake cha ITV, (Kushoto) akipokea tuzo yake.
Aidha,
tuzo hizo kwa mwaka huu zilikuwa chini ya Kamati ya TWAA ikijumuisha
Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa
Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello, Dk. Marcelina Chijoriga –
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana.
Wengine
ni Innocent Mungy – Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia
na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Kwa
upande wa udhamini ni pamoja na Delloite, TCRA, Multichoice,
Thinline,Serena Hotel, EATV na EA radio na Frontline Porter Novelli,
TSN,FPN, TEA, East Coast African Music na wengine wengi.
Mwandishi
wa Mo dewji blog, Andrew Chale (kushoto) akifuatiwa na Mkuu wa taasisi
ya Elimu ya Kimataifa ya St. Carrie’s Cente, ya Marekani Dk. Darleana
McHenry (katikati) pamoja na Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania,
Furaha Samalu. wakati wa tuzo za Wanawake Tanzania Women Achievement
Award-TWAA , Serena jijini Dar es Salaam.
Mshindi
wa tuzo ya Mwanamke wa Mwaka Mwenye mafanikio, Mkaguzi Msaidizi wa
Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia, Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca
Komba akizungumza na kituo cha TV cha East Africa mara baada ya kutwaa
tuzo hiyo.
Rais wa Vikoba, Mama Devotha Likokola akifanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Wanawake LIVE, Joyce Kiria.
Mshindi wa Young Achievement Award akiwa anahojiwa.
Baadhi ya washindi wakiwa na tuzo zao
Post a Comment