Na Andrew Chale wa Modewji blog
Tanzania
ni miongoni mwa Taifa ambalo limekuwa likikua kila kukicha kwa kila
Nyanja ikiwemo Elimu, biashara na Uchumi wake kwa ujumla ambapo mbali na
vitu hivyo pia suala la michezo ikiwemo mchezo wa mpira miguu ama soka,
umekuwa na mageuzi yake pia.
Tukija
katika suala hilo la mageuzi katika soka, ni pamoja na matumizi yake ya
nyenzo zilizokuwa zikitumika, ikiwemo mpira katika dimba. Enzi hizo
mpira uliokuwa ukitumika ni wa kufuma na makaratasi ambao ni maarufu
kama mpira wa Makaratasi au ‘Chandimu’.
Mpira
wa Chandimu umekuwa ukichezwa kwa miaka mingi sana, ambapo kwa mujibu
wa watu waliokua wakicheza miaka ya nyuma ya mwishoni mwa miaka ya 1970
hadi 80 na 90 wengi wao walikuwa wakichezea mpira huo wa Chandimu.
Pia
karibu wanasoka wengi waliowika miaka ya 1990 hadi 2000, walikuwa
hodari katika soka la mchangani ambalo asilimia kubwa walikuwa wakitumia
mpira wa Chandimu.
Hali
ya hatua hii ya kuchezea mpira wa Chandimu, inaenda sanjari na hatua ya
mwanafunzi mdogo shuleni katika darasa la kwanza hadi la tatu kuwa
ambaye anatumia penseli kuandikia kazi zake, lakini endapo atakuwa ana
akili nyingi na pia mwandiko wake ni mzuri, basi mwalimu humbadilishia
kutoka hatua ya kuandikia penseli hadi kuandikia Peni.
Mfano
mzuri mimi ninayewachambulia hapaa: Nilipokuwa darasa la tatu, Mwalimu
alinihitaji kutumia peni kwani mwandiko ulikuwa ni mzuri sana
nilifurahia katika hatua hiyo kwa mwalimu wangu huyo wa somo la
Kiswahili la kunitaka kutuimia peni, kwa tukio la kuacha kutumia penseli
na kuanza kutumia peni, nililifurahia sana kwa upande wa darasani,
Lakini nilikuwa nachukia sana kwa upande wa michezo kwani nyumbani
nilikuwa nacheza mpira wa makaratasi kwa timu ya watoto vijana wenzangu,
wakati huo huo watoto vijana wengine waliokua hodari wa kucheza mpira
wao walikuwa wakichezea mpira wa ‘gozi’ yaani mpira wa kisasa wa
kununuliwa dukani.
Suala
hili liliniuma sana hivyo nilikuwa nikijitahidi kucheza mpira mzuri ili
tu niweze kuchaguliwa kwenye timu ya wakubwa na mimi nichezee ‘gozi’
niachane na Chandimu.
Kwa
hali hiyo kutoka matumizi ya Chandimu yaani mpira wa Makaratasi kwenda
kutumia gozi yaani mpira wa dukani, ilikuwa na changamoto nyingi sana
kwani uwezo wako ndio unaohitajika kukutoa hatua moja hadi nyingine ni
sawa mfano huo hapo wa kutumia penseli na kisha ukiwa na mwandiko mzuri
na bila kufuta futa unahamishiwa kuandikia peni.
Hii
ni dondoo tu kuhusiana na mpira huu wa makaratasi au Chandimu, ambao
pia ilikuwa ukitoa ajira mbalimbali kwa watoto kipindi hicho kwani
nakumbuka hadi mimi mwenyewe niliwahi kuwa mfumaji mzuri wa mipira hii.
Nakumbuka tulikuwa tunaenda Kariakoo jioni kuokota kamba na mifuko
ambapo tukirejea na mirundo ya mifuko aaaaah ukija kufuma mpira unapata
mpira mmoja tu ama miwili.
Unayopaswa kujua mengine.
Mfuma mipira wa Chandimu lazima apangwe hata kama hajui kucheza mpira.
Ukiwa
unapiga ‘madochi’ sana yaani unapiga mashuti kwa kutumia dorl gumba
lazima utakuwa unatengwa kwani unatoboa/unafumua mipira.
Mipira
hii asilimia kubwa ilikuwa ikichezewa barabarani, wakati huo kwenye
barabara za mitaa huku kama ni uwanja basi si uwanja wote ukiwa mkubwa.
Mpira wa Chandimu ukichakaa ndio unakuwa mzuri tofauti na ulivyokua mpya.
Unakumbuka nini.
Post a Comment