Waasi nchini Sudan Kusini wamewaachilia huru wanajeshi watoto wapatao 250 .
Ni oparesheni ya tatu katika msururu wa hatua zilizoanza kuchukuliwa na jeshi hilo mnamo mwezi Januari.
Mpango
huo unatokana na makubaliano ya amani yaliotiwa sahihi mwaka uliopita
kati ya serikali na waasi katika jimbo la Jonglei wanaojulikana kama
Kobra.
Shirika la watoto la umoja wa mataifa UNICEF ambalo
linasaidia katika operesheni hiyo limesema kuwa watoto wengine 400 zaidi
pia wataachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo na kuifanya
kuwa idadi kubwa ya watoto wanajeshi walioachiliwa kufikia sasa.
Hatahivyo
UNICEF limesema kuwa kuna takriban wanajeshi watoto 12,000
wanaohusishwa na mzozo unaondelea kati ya serikali na waasi wanaoungozwa
na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.(bbc)
Post a Comment