Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji
Joseph Warioba, ametaja sifa za rais ajaye kuwa ni uzalendo, uadilifu na
dira katika kuliongoza taifa.
Jaji Warioba alisema hayo juzi, katika Kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa hewani na ITV.
“Rais anapaswa pia kujua matatizo ya Watanzania,
awe mzalendo, mwadilifu na aone mbali. Anapaswa pia kujua atafanya nini
kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta za afya na uchumi,” alisema.
Kwa kauli hiyo, Jaji Warioba anaungana na viongozi
wengine kadhaa waliowahi kuzungumzia sifa za rais ajaye, akiwamo
aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Hassy Kitine;
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye; Mwanasiasa mkongwe,
Cleopa Msuya; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba; na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao
walitaja sifa hizo za rais ajaye kuwa ni uadilifu, busara, uzalendo,
uwezo wa kufanya uamuzi na kuyasimamia, weledi wa masuala ya maendeleo,
kutokuwa na makundi, kuwa na nguvu ya mwili na akili na uwezo wa
kusimamia Katiba na sheria za nchi.
Walisema yeyote asiyekuwa na sifa hizo, hafai kuwa rais na kuwaongoza Watanzania.
Dk Kitine: Urais siyo lelemama
“Mtu anayetangaza (mwenyewe) kuwa anataka kuwa
rais anakuwa hajui anachokisema..., anakuwa hajui matatizo ya urais. Mtu
asiyejua matatizo ya urais anaweza kujisemea tu kwa sababu haelewi
urais maana yake ni nini,” alisema aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa na Waziri wa kwanza wa Ofisi ya Rais (Utawala Bora),
Dk Hassy Kitine.
Kitine alisema hayo Septemba 9 mwaka jana.
Alisisitiza, “Mtu anayejua maana na changamoto za urais hawezi kutangaza
anautaka urais. Ataogopa kwa sababu ya changamoto (nyingi) za urais…,
kwa hiyo hawezi kujitangazia ovyo kuutaka.”
Kwa mujibu wa Dk Kitine anayetaka kuwa rais
lazima awe mwadilifu wa asili na siyo wa kujifanya. Awe pia mzalendo na
mwenye uwezo wa kufanya uamuzi.
“Rais awe amesoma na asiwe na kundi, pia ajue
misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na aonekane kuwa anachukia
rushwa kwa vitendo.
Kauli ya Msuya - Mwananchi

Post a Comment