LEO hii kwenye Live Chumba cha Habari cha Global Publishers tunaye
mwanadada muimbaji anayefanya vizuri katika soko la muziki wa Hip Hop,
Witness Mwijage ambaye alikuwa akiunda Kundi la Wakilisha kipindi cha
nyuma ambapo aliambatana na mzazi mwenzie msanii wa Bongo Fleva, Ochu
Sheggy.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Witness Mwijage (kushoto), akiwa katika pozi na mchumba wake Ochu Sheggy.
Katika mahojiano na safu hii ambayo huwa inarushwa kupitia Global Tv
Online kwenye Kipindi cha Mtu Kati, Witness alisema kwa sasa yeye na
mzazi mwenzie wameunda kundi lao linalojulikana kwa jina la Ochuness
ambalo ni muunganiko wa Ochu na Witness (ness) na kuongeza kuwa
amejifunza kuimba.
Mwandishi: Witness nini kilisababisha kundi lenu la Wakilisha
kuvunjika?Witness: Kundi letu lilikuwa na watu watatu nikiwemo mimi,
Sarah Kaisi ‘Shaa’ na marehemu, Langa Kileo, kilichotufanya
tukasambaratika ni kutokana na menejimenti tuliyokuwa nayo ya Coca Cola.
Wale walikuwepo hapa nchini wakitokea Afrika Kusini ambapo lengo lao
lilikuwa kuondoa vijana wa mitaani na kuinua vipaji vya wanamuziki
wachanga. Muda wao ulivyokwisha na mkataba wetu kama washindi ukaishia
pale.
Mwandishi: Ulikutana na mzazi mwenzio, Ochu katika mazingira gani?
Witness: Tulikutana katika mazingira ya studio lakini kabla ya hapo Ochu aliniambia alikuwa akiniona kwenye runinga katika mashindano ya Coca Cola Pop Star na aliwahi kumwambia mama yake kuwa ipo siku atakuja kunioa, lakini tulikuja kukutana tena studio kwa mara nyingine baada ya miaka mingi kupita ndiyo tukawa wapenzi na mpaka leo hii tunaishi pamoja kama mke na mume japo hatujafunga ndoa.

Mwandishi: Vipi, mipango yenu kuhusu ndoa?
Ochu: Siwezi kufunga ndoa kabla sijajikamilisha kimaisha, mfano kuna vitu vyangu mimi navihitaji naomba Mungu pia huenda visipatikane sasa nitakaa bila kuoa, itanibidi nioe lakini mtu anapoamua kuoa ina maana tayari ameshajipanga na ana kila kitu sasa unakuta mtu anakuletea zawadi ya kabati au sofa hawazi kama kuna maisha mengine baada ya ndoa, angalia ndoa iliyofungwa baada ya mwezi mmoja utakuta wanandoa wamefulia.

Mwandishi: Sasa hivi mmeamua kufanya kazi pamoja ni changamoto gani ambazo mnakumbana nazo?
Witness: Tunapotaka kwenda kwenye shoo yoyote ile huwa tunakumbushana kuwa huko tunakokwenda anaweza akatokea mtu wa namna hii au ile kwa sababu tu hajawahi kukuona laivu huwa anakuona kwenye runinga basi anaona pale ndiyo mahali pa kumalizia dhamira yake.

Ochu: Menejimeti wanazopata watoto wa kike haziwi kikazi zaidi ndiyo
maana unasikia meneja kamfukuza msanii kwa sababu tu siku mbili, tatu
simu za mambo mengine nje ya muziki zilizidi na siyo muziki tena.
Nakumbuka kuna siku ilitokea nikiwa jukwaani ghafla mdada mmoja alipanda
na kuanza kunishikashika mara mabusu shingoni nikaona mama (Witness)
hanipi ushirikiano tena kama ilivyokuwa mwanzo matokeo yake akabaki kuwa
mlinzi tu.
Mwandishi: Hivi sasaw tunawaona mmekuwa kitu kimoja (Ochuness). Je,
mnatarajia kuja kuwa na meneja katika kazi zenu?Witness: Ni kweli sasa
hivi tunafanya kazi pamoja kama kundi lakini kwenye suala la menejimenti
tunajimeneji wenyewe katika kundi letu la Ochuness lakini kama kuna mtu
anataka kunimeneji mimi Ochu ruksa.
Post a Comment