MREMBO mmoja aliyejulikana kwa jina la Mariam Moshi (23), mkazi wa Mwananyamala Ujiji, aliponea chupuchupu kuuawa na wagonjwa wenye hasira kali waliolazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar baada ya kudaiwa kuiba nguo.Mariam Moshi akihamaki baada ya kukamatwa na nguo anazodaiwa kuiba katika wodi ya wazazi Hospitalini Mwananyamala.
Walinzi wa hospitali hiyo walimuokoa mrembo huyo kwa kumnasua
mikononi mwa wagonjwa hasa wajawazito walioenda kujifungua, waliodai
kwamba Mariam aliingia katika wodi yao na kuwaibia.Tukio hilo lilitokea
Machi 27, mwaka huu saa tisa alasiri, ambapo mama mmoja ndiye alishtuka
kwa kuona amechukuliwa kitenge chake kipya.
Mama huyo alipobaini ameibiwa, alitoka nje na kuangaza macho huku na
kule akiangalia alipoelekea Mariam aliyekuwa wodini kwao, ndipo
alipomuona akiwa anatoka nje kulielekea geti ambapo aliwapigia kelele
walinzi ili wamzuie.
Mariam akiwa mikononi mwa mlinzi wa hospitali hiyo.
“Walinzi walimsimamisha na kumuuliza kama aliiba kitu chochote wodini
akirudishe, lakini alikataa katakata kuhusika ma wizi huo,” kilisema
chanzo.
Hata hivyo, walinzi walipompekua, aligundulika kuwa na vitu
alivyovifunga na kufunika kwa dera (gauni kubwa, refu alilokuwa
amevaa).Askari wa kike walipomfunua gauni hilo, walimkuta akiwa na taulo
ambalo alikuwa amelifunga kiunoni pamoja na kitenge alichokuwa
akituhumiwa kukiiba wodini.
Baada ya wagonjwa kuona mali alizoiba mrembo huyo, ndipo akina mama
wengine wakiwa na watoto wao walitoka wodini na kuanza kupiga makelele
kwa hasira wakitaka apewe mkong’oto.
Walinzi hao wakitoa baadhi ya vitu alivyoiba.
Hata hivyo, walinzi wa hospitali hiyo walipoona Mariam amezongwa,
ilibidi watumie nguvu kumuokoa na kumweka chini ya ulinzi wakisubiri
namna ya kumpeleka polisi.Mariam alipohojiwa na waandishi wetu juu ya
kitu kilichompeleka hospitalini hapo, alisema alikwenda kuwaona wagonjwa
ambao hata hivyo alishindwa kuwataja. Alisema yeye ni mwenyeji wa
Dodoma anayeishi Dar kwa kujitegemea.
Aliomba msamaha kwa kitendo alichokifanya, akisema kinatokana na
maisha magumu na katika hali ya kushangaza zaidi, alipoulizwa kuhusu
taulo alilokuwa amejifunga ndani ya dera alilovaa, alisema halikuwa la
hospitalini hapo, bali aliliiba katika gesti aliyokuwa amelala siku
hiyo.
...Wakimuhoji.
Wauguzi wa hospitali hiyo walidai malalamiko ya wagonjwa kuibiwa mali
zao hospitalini hapo ni jambo la kawaida, hivyo siku hiyo ilikuwa ni
‘40’ ya Mariam.
Post a Comment