Mama wa
Mitindo Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa Fabak fashions ya Mikocheni kwa
Mwalimu Nyerer, Asia Idarous Khamsin akipita kwa madaha kwenye zuria
jekundu.
Mama
wa Mitindo, Asia Idarous anaeleza kuwa, desturi ya kupita kwenye zuria
inampa muhusika kujiamini hasa akiwa kwenye muonekano wa aina yoyote
ile. Hali hiyo imepelekea ‘event’ nyingi zinazofanyika hapa Nchini na
nchi zingine kuwa na utaratibu maalum ikiwemo kupamba eneo la kuingilia
ili wanaohudhulia tafrija ama tukio maalum kupita hao na kupata picha
ya ukumbusho.
Hata
hivyo Modewji blog, imekuwa ikifanya utafiti kwa muda mrefu ambapo
imebaini kuwa wengi wa watanzania wamekuwa hawana desturi ya kupata
‘ukodaki’ yaani picha ya ukumbusho katika shughuli wanazohudhulia.
Licha
ya kuwa wapo wanaopenda kupata picha kwenye zuria jekundu ‘red carpet’
bado muhitikio ni mdogo hasa kwa watanzania ambao wengi wao wamekuwa na
hofu ya hali ya juu bila kujua wanachoogopea pindi wanapopita kwenye
zuria jekundu kiasi kwamba mtu anayepiga picha hadi amlazimishe ama
amlainishe kwa maneno matamu ndio utakuta anakubali kupiga picha hiyo ya
ukumbusho.
Meneja wa Bang Magazine Emelda Mwamanga akipata picha na mama Wa Msanii Toka Marekani Yvonne Sangudi Kwenye Red Carpet.
Vitu ambavyo Modewji blog imevigundua
Wengi
wa wanaohudhulia shughuli mbalimbali wamekuwa na ‘tabia’ ya kuongopa
kuwa nimelala!,ama nipo sehemu fulani kumbe si kweli hayupo huko.
Pia
inaelezwa kuwa, wapo baadhi ya wanaume ama wanawake ‘kujiachia’ na
wenza ambao si wao hivyo pindi atakapopigwa picha akiwa na mwenza
aliyefika naye hapo ni sawa na kujichongea.
Utafiti
mwingine uliobainika ni kuwa baadhi yao kupita kwenye zuria jekundu na
kupiga picha wanajihis kama hawajapendeza hivyo kujiona kama wao si
lolote. Hii imekuwa ikiwakuta watu wengi sana lakini kwa hali ya kawaida
halina nguvu sana kwani Mwanadada Siyani Fadea anayefanya shughuli za
kusimamia shughuli za upambaji kwenye matamasha makubwa kwa Bara la
Asia, kwenye makala yake moja alibainisha kuwa, red carpet imekuwa
ikimpa mtu ujasiri mkubwa kwani asilimia kubwa baadhi ya mitindo,
hutokea kupitia red carpet.
“Hivyo
ambavyo unavyojiona umetoka nyumbani na kujiamini, basi ujasiri huo
ndio unaokupa nguvu na haki ya kuwa bora zaidi ya wengine hasa
unapopita kwenye zuria jekundu na kupiga picha kwenye wingi wa kamera
na mastaa” alibainisha Siyad Fadea.
Siyadi
Fadea alibainisha kuwa, ‘red carpet’ ni tukio muhimu na ambalo
linatokea mara moja tu hivyomtu unapokuwa kwenye tukio na kuna red
carpet basai ni muhimu wa kupata picha ya ukumbusho na pia ni
kumbukumbu ya mwandaaji wa tukio kuona ni jinsi gani alivyoungwa mkono.
Dondoo zingine:
Wengi
wa wandaaji wa shughuli ambazo zinakuwa na tukio la ‘Red Carpet’
wamekuwa wakijitahidi kugharamia kwa gharama kubwa ikiwemo kukodisha
‘zuria hilo jekundu’, Pia vifaa kama taa mbalimbali kwa ajili ya
kukufanya uwe ang’avu, gharama ya za kukodisha vitendea kazi ikiwemo
kamera na vinginevyo sidhani kama mtu kweli unakwepa kupita kwenye red
carpet.
Wapiga
picha: Kwa kawaida wapiga picha wanaopiga picha za matukio asilimia
kubwa wanakuwa ni wale waliopewa haki miliki na mwandaaji wa tukio, pia
shughuli zingine wapiga picha maalum ambao wao kazi yao ni kupiga na
kusafisha hapo hapo ambazo unazipata picha zako baada ya kuisha kwa
shughuli, wapiga picha hawa pindi kama picha yako ujaikomboa/kuinunua
basi picha hizo ufutwa na kutengeneza picha zingine..
Aidha,
kwa sasa licha ya wengi kuogopa kupita kwenye red carpet, suala la
mitandao ya kijamii hasa Instagram na facebook, imekuwa chachu ya wengi
kuanza kuibuka kwa kasi kupiga picha ili kutupia kwenye kurasa zake hizo
za kijamii.
Rio Poul ‘The Stylish akiwa kwenye red carpet na rafiki yake ambaye naye ni mtaalamu wa kupangilia mavazi kwa models.
Msanii
Diamond Platnumz alipokuwa Marekani alipata kupita kwenye Red carpet
ambayo ilikuwa ni maalum kwa watu maalufu na mastaa pekee, ambapo yeye
alikuwa ni miongoni mwao hali aliyopata chansi ya kusalimiana na kupata
kuhijiwa na media kubwa za nchi mbalimbali duniani.
Wema akiwa kwenye ‘red carpet’.
Mr Flavour na kampani yake wakipita kwenye red carpet kwenye tuzo hizo.
Kwa
leo, niishie hapa ila nitakuja na kingine Jumapili Ijayo: Kama una picha
ama habari ya tukio lolote lile, basi tupigie 0762388056 au Whatsapp
0762388056 ama kupitia email na namba ya simu iliyopo hapo juu.
Post a Comment