BWANA HARUSI AZIMIA MARA 3

Nivigumu kuamini! Bwana harusi Abasi Khamis Abdallah amejikuta akizimia zaidi ya mara tatu baada ya kubaini kuwa, bi harusi, Fatuma Salum Omar aliyefunga naye ndoa ni mke wa mtu na ana watoto wanne, Amani lina mkasa kamili.
Tukio hilo la kihistoria lilijiri hivi karibuni, Kigamboni, Dar mara tu baada ya ndoa hiyo kufungwa msikitini ambapo wazazi wa bwana harusi ndiyo waliotonywa kuhusu siri hiyo.
Bwana harusi Abasi Khamis Abdallah na bibi harusi wakiwa na nyuso za furaha siku ya ndoa yao.
Awali, kabla ya ndoa, wazazi wa bwana harusi walimchunguza Fatuma, akawaambia yeye bado ana ‘usichana’ wake hali iliyowaridhisha kuwa wamepata mkwe bora. Simulizi hiyo ya aina yake ilieleza kwamba, Fatuma na Abasi walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2013 bandarini jijini Dar ambapo mwanamke huyo alikuwa akitoa mizigo, wakazama kwenye mapenzi.
Ilielezwa kwamba, Abasi alimuomba Fatuma wafunge ndoa lakini mwanamke huyo aliomba apewe miaka miwili akidai kwa wakati huo anasoma kidato cha pili.Miaka miwili ilikatika huku wawili hao wakiwa kwenye mapenzi, Abasi akijua kuwa ‘mtu’ wake anamalizia masomo.Hata hivyo, ilipofika siku ya matokeo ya kidato cha nne, Abasi aliomba kujua  matokeo na kuhoji mbona haoni jina lake (Fatuma)!!
Ilidaiwa kuwa, Fatuma alimzuga kuwa alikatiza masomo dakika za mwisho hivyo dada yake akampeleka chuo.
Siku ya kupeleka posa ilipofika, Abasi alimuomba Fatuma ampeleke kwa wazazi wake, akamwambia awasiliane na dada yake, kumbe  Fatuma alimpa  dada feki ambaye aliongea na Abasi na kumwambia ampe siku mbili.
“Zilipita siku kama nne, tukamtafuta tena Fatuma na kumwambia aseme kama hataki ndoa kwani siku zinaenda na watu wameshajipanga na dada hajasema chochote, akajibu atatupeleka kwa shangazi yake ambaye anakaa Kigamboni (Dar).
Wakimeremeta siku ya harusi yao.
“Siku iliyofuata, akampeleka Abasi kwa shangazi yake, uamuzi ukatoka kuwa mahari ipelekwe Mburahati (Dar) kwa shangazi mwingine.“Mahari ilipelekwa ambapo walitaka shilingi laki saba, zikatolewa shilingi laki tano kisha laki mbili tukaahidi kumalizia siku ya ndoa.
“Cha kushangaza siku ya ndoa haijafika, tukapigiwa simu wakiomba ile fedha iliyobaki (laki mbili) itumwe kwa huduma ya mtandao wa simu, wakasumbua sana kisha tukaituma,” alisema mama wa Abasi aliyejitambulisha kwa jina moja la Fauzia .Siku ya ndoa ilipofika, Abasi na ndugu zake walikwenda kuoa, cha kushangaza walipokuwa
njiani waliambiwa waende msikitini ingawa kuna watu waliokuwa wameshatangulia nyumbani, wakadai kuwa hakukuwa na dalili ya mtu kuonesha kuwa kuna sherehe.Walipofika msikitini, Mburahati walifunga ndoa ingawa shehe alitia shaka na kumuuliza Fatuma kama ni mjane kwani wapo watu waliomtonya kuwa ni mjane.
Fatuma alikana si mjane, ndoa ikafungwa kwa shaka huku shehe akiendelea kujiridhisha.
Fauzia alisema kuwa baada ya ndoa, watu walitimba Kigamboni kwa ajili ya sherehe ndipo baadhi ya waalikwa waliporopoka kwamba, Fatuma ana watoto wanne na ni mtalaka aliyeachwa siku sita zilizopita hivyo bado yupo eda.
Kikao cha familia kilipokaa, mume wa Fatuma (baadaye iligundulika jina lake ni Asha) wa kwanza aliyejulikana kwa jina moja la Masoud alifika na kukiri kuwa alimuoa Fatuma na amezaa naye watoto wanne.
Shehe aliamuru kuvunjwa kwa ndoa ya Abasi na Fatuma ndipo bwana harusi akazimia tena, alipoamka na kuuliza mkewe yuko wapi, akaambiwa kilichotokea, akazimia tena.“Hali ya kuzimia ilitokea kama mara tatu na mara ya mwisho alipoamka alikuwa bubu, tukalazimika kumwita shehe amsomee dua ndipo akaanza kuongea,” alisema Fauzia.
Fauzia alisema harusi hiyo imewagharimu zaidi ya Sh. milioni 7 hivyo ni kitendo ambacho hawatakisahau na wanaomba watu waijue habari hii ili iwe fundisho kwa wengine.

Post a Comment

Previous Post Next Post