MASTAA wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ na Sabrina Rupia
‘Cathy’ walinaswa wakishindana kuyakata mauno vilivyo katika sherehe ya
kibao kata kiasi ambacho wahudhuriaji wote walipata wakati mgumu kuamua
nani mshindi kati yao.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa
Mango Garden jijini Dar es Salaam ambapo wasanii hao walikuwa wamekwenda
kwenye sherehe ya Kibao Kata iliyokuwa imeandaliwa na msanii mwenzao,
Vanitha Omary.
“Nimeshindwa kujizuia, muimbaji amenikuna na wimbo wa shabiki wa
Yanga, hapa ngoja kazi tuoneshane ujuzi wa kukata nyonga,” alisikika
Davina huku Cathy akiwa bize kuyakata mauno.
Hadi mwisho, wahudhuriaji wengi wa sherehe hiyo walisema mpambano umetoka droo maana wote ni ‘mafundi’
Post a Comment