Watu
wanaoishi Njoro Kaunti ya Nakuru, Kenya wameiomba Serikali ya nchi
hiyo kuwasaidia eneo la kufanyia mazishi kutokana na uhaba wa ardhi.
Ishu
ni kwamba kutokana na maeneo ya makaburi kutotosha watu wamejikuta
wakilazimika kuchimba makaburi yenye vina vifupi juu ya makaburi
mengine ili waweze kufanya mazishi.
“Serikali
itupatie mahali ambapo tunaweza kuzika watu wetu kwa amani.. sio
ukizika ukienda kulima unapata umefufua mtu mwingine… mnarudi mnamuweka
pembeni hata yeye hilo kaburi lilinunuliwa ilipaswa na yeye aweze
kuzikwa”– alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
Ukosefu wa ardhi ya kuzikia ni taatizo kubwa linalokumba maeneo mengi nchini humo.
Post a Comment