Exclusive gossip: Nuh Mziwanda wa Shilole, ‘achafua’ hali ya hewa kwenye mtandao wa Instagram

Nuh Mziwanda akiwa na mchumba wake, Shilole

..Maneno  ya ‘Sadd na Sadness’, ‘Women na Woman’ yamtatiza

Na Andrew Chale wa Modewji blog
Huenda hii ikawa ni tabia endelevu kwa baadhi ya mastaa wa Bongo hasa wasanii wa filamu, muziki na watu maalufu kwa kung’ang’ania kuutukuza ‘Umagharibi’, hasa kwa kupenda kutumia lugha ya  Kiingereza ambacho mara zote kimekuwa kikiwatoa jacho..
Hivi sasa Nuh Mziwanda ambaye mwenye mahusiano ya uchumba na  mwimbaji Shilole ameibua mijadara huku wengi wakimtupia madongo  baada ya kupost ujumbe aliouandika kwa kiingereza cha mtaani ambacho  vijana wa mjini wanasema  cha ‘Kuombea mma au cha kuungauunga’ kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram. (TAZAMA Sreen shot hapa chini)..
11149808_1085556938137392_5917159520963772825_o
Posti  aliyoitupia kwenye mtandao wake wa Instagram na kuzua mjadara kwenye mitandao mingine ya Kijamii ikiwemo ya Facebook,Whatsapp na Twitter na dewjiblog.com
 Hata hivyo  baada ya ujumbe huo kuutupia leo Aprili 11, majira mchana kupitia akaunti yake ya Instagram, yenye fans wake lukuki,  ujumbe huo ulitembelewa na watu wengi huku zaidi ya 2,000 waki-LIKE, Ambapo pia,  fans wake hao waliweza kuongelea ujumbe huo huku wengi wakimpiga madogo kwa lugha hiyo aliyoitumia  na baadala yake walimtaka kuwa ni bora angetupia lugha  yake ya Kiswahili.
Hata hivyo ni nadra sana kwa mastaa wa Bongo ama watu maalufu kujibu  komenti za fans wao, lakini kwa hili la Mziwanda lilimshinda aliamua kuwajibu wote waliompiga madongo kwa kiingereza chake hicho huku akikitetea. (TAZAMA screen shot hapa chini).
11137120_10206288399997034_3148340188159438295_n
Posti yake ya kujitetea ambayo nayo mpaka muda huu tunakuwekea hapa tayari imepata  LIKE zaidi ya 1800 na komenti zaidi ya 250 huku wengi wakimsahihisha na wengine wakimtaka aende akasome english course.
Licha ya kuwajibu huko  ni sawa kama amezima moto kwa kutumia petrol kwani walimshambulia vikali huku wengi wakimtaka aende darasani akasome kiingereza.
Tuendeleee kushirikiana nanyi marafiki wetu katika kuboresha mtandao wetu huu bora wa habari moto moto kila siku, kila saa muda wote KUWA NASI, PERUZI NASI. Tutumie habari, Picha na jambo lolote lile kupitia namba za simu zilizopo hapo juu kulia ama kupitia namba hizi 0719076376 au 0754940992
!!! Kama una Gossip !!!Exclusive tuma Whatsapp 0767076376

Post a Comment

Previous Post Next Post