Tukio
hilo lilitokea Aprili 18, mwaka huu, maeneo ya Mkuranga mkoani Pwani
ambapo awali familia hiyo ilipata taarifa kuwa kuna watu wanaonekana
kwenye shamba lao wakikata miti na kujipimia maeneo, hali iliyowalazimu
kufunga safari ili kujua watu hao walikuwa na lengo gani.
Akizungumza na waandishi wetu, Karim alisema kuwa akiwa shambani hapo
na mkewe pamoja na marafiki wengine wawili, watu hao waliotajwa kama
wavamizi waliwafuata na kuwauliza walifuata nini shambani kwao huku
wakiitana kwa miluzi, kitendo kilichowafanya waongezeke na kuwazunguka
huku wakiwa na mapanga, fimbo na visu ambavyo vilitumika kuwapiga navyo.
“Walikuwa si chini ya 30, walitupiga sana na mabapa ya mapanga
wengine kutukata nayo baadaye wakapekua mifukoni na kutulazimisha kuwapa
vitambulisho vyetu. Walitupokonya na fedha kiasi cha shilingi
780,000/= ambazo zilikuwa nyumbani kwangu,” alidai Karim.
Naye mke wa Karim aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Omary, alisema
kuwa yeye na mfanyakazi wake walivamiwa wakiwa ndani ya nyumba yao
iliyopo hukohuko shambani ambapo wavamizi hao walikuwa wakiongea Kikurya
na kuwataka wafungue mlango ambao waliufungua baada ya kutishiwa
kuuvunja.
“Baada ya kufungua walianza kutupiga kwa mabapa ya mapanga na
mwenzangu walimkata mkono, wenyewe walidai shamba hilo ni la ndugu yao
na siyo letu, nilipowabishia kwa ushahidi walizidi kutupiga na wakapekua
na kutupokonya simu zetu na fedha tulizokuwa nazo, kama hiyo haitoshi
walianza kutudhalilisha.
“Baadaye nilimuona mume wangu na wenzangu wakiletwa wakiwa wameloa
damu. Wakasema watatuchoma moto na wakachukua petroli na kuanza kumwaga
ndani, lakini rafiki yangu niliyeenda naye alikuwa ni Mkurya; akaanza
kuwaomba kwa lugha ya kwao lakini hawakumuelewa,” alisema Aisha.
Aliongeza kuwa baadaye mmoja wao aliwaambia wenzake wawatoe nyumbani
hapo na kuwataka wasirudi tena katika eneo hilo ndipo walikwenda Kituo
cha Polisi cha Vikindu na kupewa hati ya kuwawezesha kutibiwa (PF3) na
likafunguliwa jalada la kesi lililosomeka VK/RB/280/15 KUTISHIA KUUAWA
KWA SILAHA na baadaye Kituo cha Polisi cha Mbagala, Kizuiani Dar ambapo
walifungua jalada la kesi MBL/RB/3805/2015 KUJERUHI.
Akizungumza na waandishi wetu, Afisa
iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiio kwa
tukio hilo na kuongeza:
“Tayari jeshi la polisi limeshachukua hatua kwa kwenda eneo la tukio
na hali ya eneo kwa sasa imekuwa shwari kwa kuwa kuna baadhi ya watu
tayari wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo.”
Post a Comment