Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemwandikia barua Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtaka afike mbele ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa mahojiano.
Inaelezwa kuwa Makonda alimtumia Askofu Gwajima barua hiyo Machi 30 mwaka huu, akiwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa kiroho amegoma akisema hawezikwenda ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya kwa mahojiano.
Mmoja wa wasaidizi wa Askofu Gwajima amesema kuwa hatua ya Makonda kumtumia barua haikumpendeza kiongozi huyo wa kanisa.
Mmoja wa wasaidizi wa Askofu Gwajima amesema kuwa hatua ya Makonda kumtumia barua haikumpendeza kiongozi huyo wa kanisa.
“Makonda
alikuja katika Hospitali ya TMJ na kudai amekuja kumwona Askofu Gwajima
huku akiwa amebeba barua yake. Baada ya kumwuliza hali ya maendeleo ya
afya yake alitoa barua na kumkabidhi jambo ambalo halikuwa jema.
“Baada
ya muda Askofu Gwajima alituita wasaidizi wake na kutueleza kuwa
amepewa barua ya wito kwa DC, sasa tukajiuliza askofu anaumwa. Je,
inakuaje aende tena katika mahojiano na mkuu wa wilaya?
“Na kama ni hivyo nini kazi ya polisi maana wamemuhoji tangu siku ya kwanza baada ya kumkamata.
"Je,
inakuaje tena Makonda alete barua ya kumtaka askofu akahojiwe tena
mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya mbele ya DC?
“Hapa kuna mchezo unataka kufanywa na je, katika masuala haya ya usalama sijui kama huyo DC anajua wajibu wake.
“Hapa kuna mchezo unataka kufanywa na je, katika masuala haya ya usalama sijui kama huyo DC anajua wajibu wake.
"Mtu anahojiwa na polisi sasa inakuaje tena aitwe na DC ahojiwe na kamati ya ulinzi? Amesema hatokwenda,” alisema msaidizi huyo wa Gwajima.
Mwandishi
wetu alimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kupata
ufafanuzi wa barua yake hiyo, ambapo alijibu kwa kifupi kuwa ni kweli
amemwandikia barua ya wito kiongozi huyo.
Alipoulizwa ni hatua zipi Askofu Gwajima atachukuliwa kwa kutaa kutii wito huo, Makonda alisema. “Kuhusu hatua subirini mtaziona wenyewe”alisema mkuu huyo wa wilaya.
Post a Comment