Kwa muda mrefu habari za uhusiano wa mapenzi baina ya watu
mashuhuri wakiwamo wafanyabiashara na wanamuziki zimekuwa zikitikisa
vichwa vya habari katika mitandao ya kijamii, redio lakini pia hata kwa
wapenzi wa wadau hao.
Hii ni kutokana na uwazi waliouweka wahusika,
lakini pia inatokana na jinsi wanavyoivutia jamii yao kila wanapotokea
mbele za watu na kwa matendo yao.
Wapo ambao wameshatangaza kufunga ndoa pia wapo
waliopo katika uhusiano kama wachumba ambapo wametangaza kuvalishana
pete pia wapo ambao hawajafikia hatua hizo.
Mwandishi wetu wiki hii ameliangalia kwa kina
suala hili na akatoka na orodha ya couple sita ambazo zimekuwa gumzo
miongoni mwa mashabiki kiasi cha kuunda makundi katika mitandao ya
kijamii kwa kipindi cha miezi mitano iliyopita.
1. Nuh Mziwanda na Shilole
Wote ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya na kwa
kiasi fulani muziki wao ni kama unafanana. Mara kwa mara hualikana
jukwaani kufanya kazi pamoja pindi wanapokuwa na muda.
Uhusiano wao ulianza kama utani, watu walikuwa hawaamini lakini uthibitisho ulikuja kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Huko ndiko Shilole mwenyewe alikiri kwamba wao ni
wapenzi. Kuna mengi yanatokea, wanagombana na kutupiana maneno huku
Shilole mara kwa mara akimpiga mpenzi wake huyo lakini mpaka leo wapo
pamoja kama pacha.
Huku mtaani tena ndiyo shutuma za kwamba Shilole ni mkubwa kwa Nuh na kwamba kipato ndiyo kinamuweka Nuh kwa Shilole.
2. Vanessa Mdee & Jux
Hawa nao pia wanafanya muziki wa R&B,
wameshirikishana kwenye kazi na huko ndiko inasemekana walikoanzia
uhusiano wao ambao mpaka leo. Hata hivyo, ni Jux pekee aliyewahi kusema
bayana kwamba kuna kitu kati yao.
Hata hivyo, uhusiano unaonekana dhahiri, kila
mmoja humuongelea vyema mwenzake na kila mmoja anafanya kazi nzuri kwa
hiyo wamejikuta wakipeana mashabiki kila mmoja kutokana na umaarufu
wake.
- Mwananchi
Tetesi za mtaani zinasema huku pia kuna tofauti kubwa ya umri
kati ya Vanessa na Jux lakini kingine pia ni kwamba Jux anadaiwa kuwa na
kipato kikubwa kuliko Vanessa.
Kingine ambacho kinaleta minong’ono ni hatua ya
Jux kuamua kummwaga mpenzi wake, Jack Cliff baada ya tuhuma za kushikwa
na dawa za kulevya nchini China na kuamua kutoka na Vanessa.
3. Faraja na Nyalandu
Hapa unamzungumzia wanandoa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu na mrembo aliyeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya urembo ya dunia mwaka 2004, Faraja Kotta uhusiano wa
wanandoa hawa umeingia katika minong’ono baada ya Nyalandu kutuhumiwa
kuwa na uhusiano na msanii mwenye mvuto wa tasnia ya filamu Tanzania,
Aunt Ezekiel.
Wengine wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa hata ujauzito aliokuwa nao mwanadada huyo ni wa mheshimiwa huyo.
Kila mtu alisema lake lakini katika ufafanuzi
ambao ulitoka pande zote mbili ni kwamba kama kwa njia moja au nyingine
kuliwahi kuwa na uhusiano kati ya hawa wawili, ulikuwa ni wa kikazi.
4. Zari & Diamond
Kwa sasa couple hii ndiyo gumzo la mjini. Daimiond
ambaye jina leke halisi ni Nasib Abdul ni kijana aliyewahi kuwa muuza
mitumba na ghafla akaitafuta njia ya kutoka kimaisha kupitia muziki.
Bahati ikamdondokea na sasa kijana huyo ametulia kwa mwanamama wa
Kiganda anayedaiwa kuwa na mkwanja mrefu zaidi ukilinganisha na wanawake
wengine nchini mwao.
Mara ya kwanza ilionekana kama kuna mradi
wanauhangaikia pamoja, lakini ghafla ikaja kugundulika kwamba ni watu
walio katika mapenzi mazito tena wanaotegemea mtoto hivi karibuni.
Zarina ana watoto watatu tayari ila Diamond bado
ni kijana mdogo kiumri ukilinganisha na mwanamama huyo. Minong’ono
inazidi kila kukicha katika mitandao ya kijamii na mashabiki wa karibu
wa mwanamama huyo hawaamini kama ni mjamzito hali iliyosabisha kuamua
kupiga picha tumbo lake na kuweka katika mtandao wa Instagramu.
5. Ray Kigosi na Chuchu Hans
Kati ya uhusiano ambao ulipokelewa kwa hisia
tofauti miongoni mwa mashabiki wa tasnia ya filamu ni huu, maana hakuna
aliyewategemea kabisa.
- Mwananchi
Post a Comment