Kufuatia
idadi kubwa ya Watanzania ambao mara kwa mara husafiri kwenda India kwa
sababu tofauti tofauti za kimatibabu, wataalamu kutoka Hospitali ya Apollo, Hyderabad,
wamefikia uamuzi wa kutoa tiba na ushauri wa kitaalamu kwa Watanzania
kupitia kiliniki maalumu ya siku mbili itakayofanyika Dar es Salaam.
Kliniki hii maalum itaendeshwa na mtaalamu wa upasuaji wa mfumo wa fahamu, Dkt Alok Ranjan na mtaalamu wa upasuaji wa mifupa, Dkt Somasekhar Reddy katika hospitali ya Hindu Mandal tarehe 27 na 28 Aprili.
Timu hiyo ya madaktari wataalamu kutoka Hospitali ya Apollo itaambatana na Bw. Radhey Mohan makamu mwenyekiti, maendeleo ya biashara kimataifa katika hospitali ya Apollo Hyderabad. Tukio
hili la siku 2 itakuwa fursa ya watu wenye magonjwa yanayohusiana na
magoti, nyonga, mabega na mfumo wa fahamu kuonana na madaktari
wanaotambulika kimataifa kwa uchunguzi wa awali na ushauri.
Makamo wa rais anasema “Kwa
sasa Idadi ya Watanzania wanaotafuta huduma za afya nje na hasa India
ni kubwa, kila siku tunapokea watu wanaohitaji huduma zenye ubora wa
hali ya juu. Kuzingatia hili tumeamua kutanua wigo wetu na kufikisha
wataalamu wetu karibu na wahitaji ambao wanaweza wasipate fursa au namna
ya kuonana nao”. Kulingana na Bw. Radhey Mohan
hatua hii ni alama ya mahusiano ya muda mrefu ambayo hospitali za Apollo
zimeanzisha na Tanzania ambapo kwa miaka mingi imeshuhudia hospitali
hizi zikitoa huduma zake kwa waathirika wa magonjwa mbalimbali
yaliyokithiri nchini.
Kliniki hii
ya siku mbili itawahudumia wagonjwa mbalimbali na ipo wazi kwa kila
mmoja atakayewahi kuweka miadi; wagonjwa hawa watafanyiwa uchunguzi,
watapewa maelekezo na ushauri wa kitaalamu kwa kuzingatia matatizo
waliyonayo.
Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 25, na akiwa amekwishafanya upandikizaji wa viungo zaidi ya mara 1,000, Dkt Somasekhar Reddy, Mshauri mwandamizi wa upasuaji wa mifupa, Hospitali ya Apollo, Hyderabad, atawahudumia watu wenye matatizo yanayohusiana na magoti, nyonga na mabega. Dkt Reddy
ana uzoefu wa juu katika kufanya kazi karibu zaidi na Watanzania
waliokumbwa na matatizo yaliyotajwa amekwishawafanyia upasuaji zaidi ya
Watanzania 200 katika kipindi cha miaka 7 hadi 8.
Dkt. Reddy
anaongoza timu ya wataalamu upasuaji wa mifupa ambayo inatoa huduma za
kipekee kwa matatizo yote ya mifupa na viungo katika hospitali ya
Apollo. Utaalamu wake hasa ni katika kupandikiza nyonga, goti na bega,
upasuaji wa kupandikiza nyonga, upasuaji wa goti, upasuaji usio vamizi,
majeraha katika maungio ya goti na bega pamoja na upasuaji wa kusaidia
mguu wenye saratani ya mfupa.
Atakayeambatana na Dkt Reddy ni Mkuu wa kitengo cha upasuaji wa mfumo wa fahamu katika hospitali ya Apollo, Hyderabad Dkt Alok Ranjan ambaye
kwa upande wake atahudumia wagonjwa wanaohitaji upasuaji umakini zaidi
wa mfumo wa fahamu. Ni mkongwe katika upasuaji usio vamizi wa uti wa
mgongo na saratani ya ubongo, upasuaji mdogo wa mfumo wa fahamu akiwa
ameweka rekodi ya kufanikiwa kutibu zaidi ya wagonjwa Watanzania 1,000
kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kwa matatizo magumu ya ubongo na uti
wa mgongo.
Dkt Ranjan
ni mtaalamu katika upasuaji wa fuvu lenye saratani, upasuaji tata wa
uti wa mgongo, upasuaji kwa watoto wadogo, upasuaji unaohusisha mionzi,
upasuaji wa mfumo wa fahamu ujulikanao kitaalamu kama AVM, upasuaji
kwenye ubongo kwa kutumia hadubini, upasuaji kwa wagonjwa wa kifafa na
ule wa kuusisimua ubongo.
Watanzania
wanahamasishwa kutumia fursa hii kuwaona madaktari na kupata ushauri wa
awali wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wanaotaambulika kimataifa.
Ushauri huu wa siku mbili utafanyika hospitali ya Hindu Mandal Dar es
Salaam tarehe 27 na 28 Aprili kati ya saa 3 asubuhi na saa 12 jioni. Kwa
watakohitaji kuweka miadi na madaktari wanaweza kupiga simu +255 682 052 342 or +255 22 211 499-4
Post a Comment