Cha mwisho kusikika kutoka kwenye
HEADLINES za Bungeni March 2015 ilikuwa ishu ya mjadala wa Muswada wa
Matumizi ya Mtandao, mvutano ukawa mkubwa na kusababisha Bunge
kuahirishwa saa tano usiku… Wabunge walikuwa wakivutana kuhusu kupitisha
baadhi ya vipengele kwenye Muswada huo.
Okay, n’na stori ya Kenya sasa hivi, ishu ni hiyo hiyo kesi ya matumizi ya mitandao.. Kijana mmoja Robert Mungai yeye
tayari yuko mikononi mwa Mahakama, kinachosubiriwa ni Mahakama
kuendelea kusikiliza kesi yake na kuamua hukumu pia kutokana na jamaa
huyo kukabiliwa na kesi ya kuandika ujumbe wa uongo kwenye ukurasa wake
wa Facebook siku ya April 4 2015.
Polisi Kenya wamesema Robert aliandika ujumbe wa kuwaonya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton University kilichoko Njoro, ambapo ujumbe alioandika alikuwa akiwataarifu wenzake kuwa Kikundi cha Al-Shabaab kitashambulia.
Robert alikataa kutenda kosa hilo lakini Polisi walikataa asiachiliwe kwa dhamana kwa kuwa uchunguzi bado haujakamilika.
Imeripotiwa na vyombo vya habari Kenya,
wanasema kwa Sheria ya nchi hiyo ilivyo huenda hukumu yake ikawa kifungo
cha zaidi ya miaka ishirini.
Alan Wadi Okengo aliwahi
kuingia kwenye HEADLINES pia toka Kenya January 2015 baada ya
kuhukumiwa mwaka mmoja jela na kulipa faini kwa kosa la kumtukana Rais Kenyatta mtandaoni.
Ilisikika kwenye show ya #AMPLIFAYA.. TV ya K24 waliripoti hii pia, unaweza kuisikiliza na kuangalia video yake hapa…
Post a Comment