Mahakama inayoshughulikia ufisadi nchini Bangladesh imemuachilia kwa dhamana kiongozi mkuu wa upinzani Khaleda Zia.
Zia anatuhumiwa kwa kufuja pesa za misaada wakati akihudumu kama waziri mkuu, mashtaka ambayo anasema ni ya kisiasa.
Amri ya kukamatwa ilitangazwa dhidi yake mwezi Februari kwa kukosa kufika mahakamani.
Kufika
kwake mahakamani ndiyo mara yake ya kwanza kuondoka afisini kwenye mji
mkuu wa Dhaka tangu atishie kuongoza maandamano ya kupinga serikali
kwenye mitaa ya miji wakati wa maadhimisho ya siku ya uchaguzi mkuu
uliokumbwa na utata.(BBC)
Post a Comment