Kwenye vichwa vya habari kubwa
MAGAZETINI iko iliyoandikwa ‘CHADEMA, ACT jino kwa jino’, wanazidi
kuchuana kwenye mikutano huku viongozi wake wakishutumiana, iko
iliyoandikwa kuhusu wakazi wa Hanang’ Manyara kutangaza kumuunga mkono Wakili Duncan Mayomba akigombea Ubunge kwa kuwa amekuwa akiwatetea sana wakazi wa Wilaya hiyo kwenye masuala ya Kisheria.
Afande Sele kaandikwa nae, amesema anataka kuwa Mbunge wa tofauti na sio Ubunge wa kuvaa suti na kupokea Rushwa.
Chuo cha UDSM kimeshika
nafasi ya kumi kwa ubora Afrika, Serikali imetangaza kuzifuta taasisi
zaidi ya elfu kumi za kidini na NGO ambazo zimetajwa kuvunja kanuni
mbalimbali ikiwemo kujihusisha na siasa.
Headline nyingine ni ishu ya NEC
kutangaza kuwasili mashine mpya za BVR kwa ajili ya kuandikisha
Wapigakura TZ ndani ya wiki hii, nyingine ni kuhusu Serikali kutangaza
kuwarudisha TZ watu wote walio tayari kurudi kutoka Afrika Kusini,
Kuna mahojiano pia ambapo kasikika
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambaye amesema wanaanza kupitia
mwenendo wa vyama vya Kijamii, vikipatikana vilivyokiuka kanuni na
Sheria vitafungiwa.
Uchambuzi huu bonyeza play hapa uusikilize..
Post a Comment