Hili
tukio huenda likakushtua kutokana na mazingira ambapo limetokea, sawa
tunaenda Hospitali kutibiwa lakini wale wanaotoa huduma wakati mwingine
wanakuwa na mambo yao tofauti.
Hii story unaambiwa imetokea Uingereza, Andrew Hutchinson ni nesi wa kitengo cha dharura Hospitali ya John Radcliffe Uingereza, amekutwa na hatia ya kuwabaka wagonjwa watatu walioenda kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

Hospitali ya John Radcliffe
Muuguzi
huyo anadaiwa kuwabaka wagonjwa hao waliofikishwa kwenye Hospitali
hiyo wakiwa wamepoteza fahamu, halafu akakutwa na picha na video
alizojirekodi wakati akifanya kitendo hicho.
Polisi
walipomkamata walikagua simu yake, computer na camera na kukuta picha
hizo.. Mtuhumiwa anashikiliwa na bado uchunguzi unaendelea kwani jamaa
imeonekana ana kesi pia ya kubaka watoto wawili.
Wanawake waliofanyiwa vitendo hivyo hawakujua chochote kwa kuwa jamaa aliwaingilia wakiwa hawana fahamu.

Post a Comment