NDOA YA THEA, MIKE CHALI TENA

Ndoa ya mastaa wa Bongo Movies, Michael Sangu ‘Mike’ na Salome Urassa ‘Thea’ inadaiwa kuanguka chali kwa mara nyingine baada ya mwanadada huyo kurudi kwa wazazi wake kwa muda mrefu sasa.Chanzo makini kilidai kwamba, wawili hao walitengana miezi mitatu iliyopita na Thea kurudi nyumbani kwa mama yake maeneo ya Kinondoni jijini Dar kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni migogoro ya mara kwa mara.
Mastaa wa Bongo Movies, Michael Sangu ‘Mike’ na Salome Urassa ‘Thea’ siku ya harusi yao.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu waliwaendea hewani kwa nyakati tofauti, Mike na Thea ambapo kila mmoja alifunguka kivyake. “Mh nani kawaambia maneno hayo? Watu wanapenda kuzusha sana, mimi najua mke wangu bado nipo naye amekwenda kwao kupumzika atarudi,” alisema Mike.
Kwa upande wake Thea alifunguka: “Mmh, hakuna kitu kama hicho nani aliyewaambia, Mike kama amesema nimeenda kupumzika anajua yeye, kwanza naenda kupumzika nina mimba? Mimi nilikuwa ‘production’ na hivi ndiyo narudi nyumbani nikifika nitakupa simu uongee na Mike.”Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni Thea hakuwasiliana na mwandishi ambaye anasubiri simu yake mpaka sasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post