Askari
mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria,
aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika kuuawa jana mchana na
wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya
dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.
Tukio
hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)
waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo
ni mali ya polisi.
Mashuhuda
wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda
ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu
kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.
Baada
ya kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini
wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo kumjeruhi polisi
mmoja.
Post a Comment