Sijawahi kusikia marubani wamepigana ndani ya ndege, hii imetokea India

Bado hatujausahau msiba wa ndege ya Ujerumani kuangushwa na Rubani msaidizi kwa makusudi Ufaransa na kuua zaidi ya watu 150 ndani yake, sasa tunayo hii nyingine kutoka India.
Shirika la ndege ya Air India limewasimamisha kazi marubani wake wawili baada ya kudaiwa kupigana ndani ya chumba cha Marubani kwenye ndege hiyo iliyokua na safari ya kutokea Delhi kwenda Jaipur.
cockpit 
Japo shirika lenyewe linasema kilichotokea ni kurushiana matusi, habari za uhakika kwenye vyanzo vingine zimeonyesha jamaa hawa walipigana na Rubani Msaidizi ndio anadaiwa kuwa chanzo cha kulianzisha, yani Captain (Rubani mkuu) alimuagiza kurekodi data ikiwemo kufahamu ni abiria wangapi wapo ndani ya ndege kabla hawajapaa hapo ndio ugomvi ukaanzia.
Hii ishu imetokea wakati headlines za ndege 2015 zikiwa kwenye wiki yake nyingine tena toka ndege ya Ujerumani iangushwe kwa makusudi na Rubani Msaidizi March 24 2015 ambaye alimfungia nje ya chumba cha Marubani, Rubani mkuu aliyekua ametoka nje kwa wakati huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post