MKONGWE kwenye soko la ugizaji Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka
kuwa miaka ya hivi karibuni wasanii hawaishi pamoja kama zamani kwani
shetani amewaingilia katikati na kuwatenganisha.
Mkongwe kwenye soko la ugizaji Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Thea alisema kipindi cha nyuma
wasanii walikuwa waipenda sana kuwa na kundi moja wakakaa pamoja na
kuelewana lakini kukatokea kitu ambacho mpaka leo hakieleweki
wakasambaratika.“Naamini kuna vitu tulikosea, tunateseka kweli.
Tunatakiwa kabisa kumrudia Muumba wetu kwa kuwa hakuna cha Bongo Movies
wala nini na ninaona inaelekea kufa kabisa lazima tukae na kujikagua
upya,” alisema Thea.
Post a Comment