MWANADADA kutoka tasnia ya filamu na muziki Bongo,
Tiko Hassan ameikimbia nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Mwananyamala
jijini Dar kutokana na mambo ya kishirikina.Akizungumza hivi
karibuni Tiko alisema kuwa, ameamua kuihama nyumba hiyo licha ya kwamba
kodi yake haijaisha kufuatia maruweruwe yaliyokuwa yakimpata nyakati za
usiku.
Mwanadada kutoka tasnia ya filamu na muziki Bongo, Tiko Hassan.
“Yaani nimekuwa nikishindwa kulala kwa raha kwani usiku huwa nasikia
sauti za ajabu, mara nahisi kuna watu wanatembea ndani, mara mapaka
yanalia dirishani kwangu, kimsingi sikuwa nikiishi kwa amani, nimeona
nihamie Kinondoni yasije yakanikuta makubwa,” alisema Tiko
Post a Comment