Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaahirisha Kura ya Maoni Ya Katiba Mpya.....Zoezi La Uandikishaji Kuendelea Hadi Mwezi Wa 7

Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, haitaweza kufanyika tena tarehe 30 April hadi hapo itakapotangazwa tarehe nyingine tena.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  leo  mchana, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi , Jaji Mstaafu Damian Lubavu amesema sababu ya kuhairisha kura hiyo April 30 ni kutokana na kutokamilika kwa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura  kutokana na changamoto za mashine za BVR.

Jaji  Lubavu  amesema zoezi la uandikishaji mkoa wa Njombe litakamilika April 18 na baada ya hapo itafuatia mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mtwara na Lindi ‪. Vifaa vya kuandikishia (BVR kits) nyingine 248 zitawasili ndani ya wiki ijayo na vingine 1600 vitafuata baada ya muda mfupi. 
 
Pia,  amesema kama vifaa vya kuandikishia vitafika vyote zoezi la uandikishaji litakamilka ifikapo mwezi julai mwaka huu.
 
Jaji  Lubavu  ameainisha  kuwa Gharama za vifaa vyote vilivyoagizwa kwaajili ya vifaa vya kuandikishia (BVR kits) ni dola za Kimarekani milioni 72 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 13,338,520,536

Post a Comment

Previous Post Next Post