Tunda Man Afunguka Juu Ya Picha/Ujumbe Uliopostiwa Instagram baada ya kifo cha Abdul Bonge - Unaohusu show ya 254

Jana ndio mwanzilishi wa kundi la Bongofleva la Tiptop Connection Abdul Bonge amezikwa Morogoro baada ya kufariki weekend iliyopita kutokana na kuanguka vibaya alipokua akiamulia ugomvi wa jirani yake.
Dakika kadhaa tu baada ya kifo cha Abdu Bonge, msanii wa TipTop Connection Tunda Man alipost picha kwenye account yake ya Instagram akiwaambia mashabiki wake wa Kenya wakae tayari kwa show yake akisema ‘Pande za 254 kitawaka mbaya pale jamboree Mombasa, watu wa Mombasa tukutane palee

Tunda Man 1
Tunda Man akihojiwa na ripota Askofu wa TZA .

Ni post ambayo ilifanya mashabiki wengine wamtukane, wengine wamlaumu na wengine wahisi kama aligombana na Tiptop hivyo hana shughuli na yanayoendelea kwao ambapo pamoja na hayo, Tunda Man amesema wote hao hawakuwa wanaujua upande wa pili wa picha hiyo, yani kilichotokea hasa.

Akiongea akiwa analia Tunda Man amesema >>> ‘Abdu Bonge ndio aliipost hiyo picha mimi nilikua naendesha gari manake alikua anajua mimi nilikua natakiwa kwenda Mombasa wiki hii, simu haikuwa na hela kwa hiyo baadae nilipoweka pesa ndio ikajipost wakati nikitaka kuweka picha ya Marehemu, ilivyojipost ikabidi niende nikaifute nikaweka nyingine’

Tunda man 4 
Ni mtu ambae nilikua napiga nae picha nyingi na huwa anazipost mwenyewe, ana comment sababu anajua mimi ni mzembe naweza nisiwe nakumbuka kupost kuhusu kutangaza show zangu, bila Abdul Bonge sidhani kama kuna mtu angemjua Tunda Man sasa hivi

Sauti yake nyingine Tunda unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa chini



Tunda man 5

Post a Comment

Previous Post Next Post