Wafanya biashara ya ngono wakiwa kazini
Hivi
umeshawahi kujiuliza kwamba wafanyabiashara ya ngono ni watu wa namna
gani? Ama biashara hiyo ni biashara kama biashara zingine kivipi? Nchini
Australia,maelfu ya wafanyabiashara ya ngono bila soni wameweka bayana
namna wanavyotumia mitandao ya kijamii na kuueleza ulimwengu jinsi
wanavyo fanikisha biashara hiyo.
Huwa hawachagui wateja,Mwanafunzi
mwenzangu? Mwanasheria nimtakaye,mwanaharakati,binti yangu?dada yangu,
mfanya biashara mwenzangu wa ngono? Familia yangu! Sihitaji msaada wao.
Huo
ni baadhi ya maelfu ya ujumbe kutoka nchini Australia kwa wafanya
biashara ya ngono wanaojieleza huku wakitumia ukurasa wa
#facesofprostitution hashtag.Fukuto hili lilianza tangu mwishoni mwa
juma lililopita katika Instagram na mfanya biashara wa ngono mwenye umri
wa miaka 21 ambaye ni mhitimu wa masuala ya Historia anayejulikana kama
Tilly Lawless.
Aliamua kuzungumzia blog moja iliyoamua kurudia
kuweka kwenye ukurasa wake taarifa iliyorushwa wiki iliyopita katika
ukurasa wa gazeti maarufu lenye kuandika habari za akina mama liitwalo,
Mamamia.Blog hiyo iliandika katika maadhimisho ya miaka ishirini na
mitano mkutano wa wafanya biashara ya ngono na filamu yao ya
‘prince-charming Pretty Woman' na kudai kuwa shuhguli nzima ya biashara
ya ngono haina mvuto kama ilivyo katika filamu hiyo.
Tilly Lawless
alichukizwa na namna taarifa hiyo ilivyoweka mambo kirahisi rahisi na
kuijumuisha biashara ya ngono na kuiona biashara hiyo kama yenye madhara
.bibi huyo anashuhudia kuwa ameifanya biashara hiyo ya ngono kwa miaka
miwili lakini amejulikana hadharani miezi miwili iliyopita mjini
Sydney,mahali ambako biashara ya ngono ruksa kuifanya kisheria . na
alichukua maamuzi ya kuweka picha yake bayana katika ukurasa wake wa
Instagram kuonesha uzuri na upande wa pili wa biashara ya ngono ,sura ya
mwanamke mrembo,ambaye anajitambua na aliyechagua kuwa mfanyabiashara
ya ngono kwa mantiki ya kukipinga kilichoandikwa katika jarida la
Mamamia na blog pia

Post a Comment