NYOTA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ambaye
alipata ajali na kusababisha kukatwa kwa mguu wake wa kulia, juzikati
alijikuta akianguka chooni akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es
Salaam na kuumia mguu wake mzima.
Nyota wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.
Chanzo cha habari kilichokuwepo wakati wa tukio hilo, kilisema kuwa Wastara alilazimika kuchechemea kwa kutumia mguu wake
wa bandia aliowekewa, wakati akitoka ili kuwapata wasamaria wema
kuelekea hospitalini.
“Ungemuona kiukweli ungemuonea huruma kwani alijikuta akisikitika na kujiuliza kwanini amekuwa mtu wa matukio kila wakati,” kilisema chanzo chetu.Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, gazeti hili lilimwendea hewani muigizaji huyo ambaye alikiri kutokewa na tukio hilo, akisema wakati huo alikuwa njiani akielekea hospitali kwa ajili ya ‘kuchekiwa’ mguu huo kwani alikuwa akijisikia maumivu makali.
“Yaani we acha tu nashukuru ingawa nina maumivu makali kwa sasa nipo njiani naelekea hospitali kuucheki kwani ndio mguu uliobaki ninaoutegemea,” alisema Wastara

Post a Comment