Hatimaye lile sekeseke la ndoa ya meneja wa wasanii wa Bongo Fleva 
wanaosimamiwa na Kampuni ya Endless Fame, Petit Man na mdogo wa 
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz limemdondokea
 Wema Isaac Sepetu anayedaiwa kuitibua kiasi cha kuwatenganisha na kila 
mmoja kuchukua hamsini zake.

Habari kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, Wema amehusika kwa 
asilimia kubwa kutibua ndoa hiyo kwani amekuwa akimtafutia mademu Petit 
Man, jambo ambalo Esma alilishtukia na kuamua kumbwatukia Wema kwa 
kuandika maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa taarifa yenu Esma anamlalamikia Wema kuwa anamfanya mumewe kuwa 
mhuni kiasi kwamba anachukua mademu, tena marafiki zake na hata 
akimuuliza Petit Man anajifanya hao ni mashoga wa Wema.“Anapomkomalia, 
mara kadhaa umekuwa ukizuka ugomvi mkubwa na Petit Man anahama nyumbani 
kwake na kukimbilia kwa Wema,” kilisema chanzo chetu.Baada ya 
kunyetishiwa ‘infomesheni’ hizo, gazeti hili liliingia kazini kusaka 
ukweli wa mambo yanayodaiwa juu ya
lilianzia
 kwa Esma, alipopatikana alisema ni kweli hivi karibuni aliandika ujumbe
 kwenye Mtandao wa Instagram, ingawa kwenye maelezo yake hakumtaja mtu 
bali aliandika kwa hisia kama binadamu mwingine anavyoweza kuandika.
“Nani anasema nimemtukana mtu? Niliandika mambo ambayo nilijisikia 
mwenyewe lakini sikumtaja wala kumlenga mtu yeyote, kama kuna mtu 
alikwazika basi atakuwa anajichanganya mwenyewe.“Mimi sina tatizo na 
Wema na mambo ya familia yangu siwezi kumwambia kila mtu hivyo kama kuna
 ugomvi kati yangu na mume wangu hayo ni mambo ya familia yetu,” alisema
 Esma.
Kwa upande wake Wema alifunguka kwamba hajawahi kuongea jambo na Esma
 na kama kuna kitu aliandika kwenye ‘peji’ yake yeye hakuona.Alisema 
anachokumbuka ni kwamba aliongea naye (Esma) akiwa Hospitali ya Aga Khan
 Aghakan, Dar.
“Huwa siongei na Esma mara kwa mara kwani sina sababu sana ya kuwa naye kwa kuwa si mume wala bwana’ngu.“Pia sijawahi kukwaruzana naye, sasa kama kuna kitu alisema, mimi namtafutia wanawake mumewe basi atakuwa anakosea kabisa,” alisema Wema.
Post a Comment