Staa wa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu amewatolea uvivu baadhi ya
watu ambao wameibuka kwa wingi mtandaoni wakiitoa karoso miguu ya staa
huyo mara baada ya Wema kuweka picha kadhaa akiwa amevaa sketi amabayo
inaonyesha miguu yake.
“Naomba niwaulize nyinyi mnaojiona miungu watu.... Mlitaka nijiongeze
nyama miguuni kwangu au...? Ndo ilivyo na kuacha kuvaa nguo za kuionesha
siwezi... Ntavaa tu... Yaani wala siwezi acha... Iwe mibaya iwe ina
makovu iwe na michirizi ni ya Wema Sepetu... na kwakuwa ni yangu basi
nita i embrace.. Tuko pamoja eeh... Sasa muache vifimbo vyangu... maana
ndo Mungu alonibarikia navyo…” Wema ameandika kupitia ukurasa wake
mtandaoni
Post a Comment