Ufisadi! Kibosile mmoja aliyefahamika kwa jina la Mangi Pesa
amekamatwa na polisi akiwa na shehena ya vyandarua vya serikali vya
msaada ambavyo hugawiwa bure, akivitoa kwenye mifuko yake na ‘kuvipaki’
kwenye mifuko ya vyandarua vinavyouzwa.
Mangi Pesa anayedaiwa kwa ufisadi wa vyandalua.
Tukio hilo la kushangaza lilijiri Jumamosi iliyopita kwenye ‘godauni’
la jamaa huyo lililopo katika nyumba moja iliyopo Sinza C jijini Dar
kwa msaada wa taarifa kutoka kwa wasamaria wema waliochoshwa na ufisadi
huo wa Mangi.
Habari zilieleza kuwa Jeshi la Polisi kwenye Kituo cha Kijitonyama
almaarufu Mabatini jijini Dar lilipokea taarifa za kuwepo skendo hiyo
ambapo lilifika eneo la tukio mara moja kama kawaida yake na kumdaka
Mangi akiwa tumbo wazi ambapo walimng’ang’ania vilivyo baada ya kutaka
kuleta ‘rabsha’.
Mangi Pesa akiwa chini ya ulinzi.
Dakika sifuri baadaye, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers nayo ilifika eneo hilo na kumkuta Mangi akiwa chini ya
ulinzi ambapo alipokaguliwa alikutwa na shehena hiyo ya vyandarua vya
msaada.
Kwa mujibu wa wasamaria wema hao, jamaa huyo amekuwa akijihusisha na
mchezo huo kwa muda mrefu huku ikisemekana kuwa huwa anakula dili na
wahusika ambao ni vigogo serikalini wanaomuuzia kwa bei chee naye
‘kuvipaki’ upya na kwenda kuuza kwa bei ya juu.
Akiingizwa kwenye gari.
Akiwa amezungukwa na shehena hiyo kwenye godauni lake huku mzigo
mwingine ukiwa kwenye magari yaliyokuwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo,
Mangi alionekana kutaharuki kwani hakujua kama angenaswa katika
mazingira hayo.
Hata hivyo, polisi hao walimtuliza na kumpiga pingu kisha kumbeba
kwenye gari na vidhibiti vyake na kumpeleka Kituo cha Polisi cha
Mabatini kwa ajili ya upelelezi zaidi wa tukio hilo ili sheria ichukue
mkondo wake.
Baadhi ya vyandalua vilivyoibiwa na kigogo huyo.
Habari zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni
zilieleza kuwa Mangi aliachiwa kwa dhamana akisubiri kufikishwa
mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
Post a Comment