AMAZING! Hiyo ndiyo kauli pekee unayoweza kuitamka
kuakisi shoo baab’kubwa aliyoifanya mkali wa wimbo wa Nasema Nao, Nasibu
Abdul ‘Diamond’, London, Uingereza, Risasi Mchanganyiko linakujuza
zaidi.
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipagawisha wakazi wa jiji la London.
Shoo hiyo iliyoacha gumzo la aina yake nchini humo kutokana na kupata
idadi kubwa ya mashabiki, ilifanyika Jumapili iliyopita katika Ukumbi
wa Royal Regency, maeneo ya Manor Park.
Chanzo chetu kilichoambatana na msafara wa Diamond kwenye shoo hiyo
ijulikanayo kama Diamond are Forever, kiliweka bayana kuwa shoo hiyo
ilikuwa ya kustaajabisha (amazing) kwani ilikadiriwa kuwa na watu zaidi
ya 1500 ambao ni Wabongo waishio nchini humo waliochanganyika na
wazungu.
Akitambulishwa mbele ya mashabiki.
“Jamaa kapiga shoo ya nguvu, watu walijaa kweli, si Wabongo pekee
bali Wazungu nao walikuwepo. Si zile shoo za kupiga sebuleni ambazo
wasanii wengi wa Kibongo huwa wanafanya. Yani hadi leo (Jumatatu) kila
mtu anaizungumzia. Imeacha gumzo la aina yake.
“Ilikuwa yenye hadhi maana kiingilio kilikuwa ni shilingi laki moja
na ishirini kwa V.I.P na elfu tisini viti vya kawaida, Wazungu
walichanganyikiwa hadi ikabidi waulize Who is Diamond? (Diamond ni
nani?) wakaambiwa na meneja wa msanii huyo, Babu Tale kuwa ni msanii
anayeiwakilisha Tanzania akitokea Tandale, Dar es Salaam,” kilimwaga
data chanzo hicho.
Mbali
na umati huo ‘kuinjoi’ nyimbo za Diamond kama Kamwambie, Mbagala, Kesho
na Nasema Nao na nyingine kibao, shoo hiyo iliongeza msisimko kufuatia
uwepo wa balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Peter Kalaghe ambaye
alipewa nafasi ya kuzungumza machache jukwaani, burudani ikaendelea.
Post a Comment