Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim (katikati) akitoa taarifa
hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu Baraza la Wazee Taifa, Roderick Lutembeka
na kulia ni Mkurugenzi wa Bunge ndani ya Chadema Halimashauri Kuu, John
Mrema
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa taarifa yake juu ya
utaratibu utakaotumika katika uteuzi wa wagombea ndani ya chama hicho
kwa mwaka wa 2015.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
Zanzibar, Salum Mwalim ametaja mchakato wa uteuzi kuwa utahusisha hatua
tatu katika ngazi ya kata na jimbo au wilaya na hatua moja katika ngazi
ya kitaifa.
Mwalimu
alisema kuwa ngazi ya kwanza ni Mkutano Mkuu wa Jimbo ambao utafanyika
siku moja kwenye eneo moja au Makao Makuu ya Jimbo au eneo ambalo
litaamuliwa na vikao vya chama, wagombea kujipigia kura wenyewe na
kamati ya utendaji ya jimbo ambayo kazi yake itakuwa ni ya uteuzi wa
awali kwa mujibu wa katiba ya chama na kuwasilisha mapendekezo yake kwa
Kamati Kuu.
Aidha,
aliongeza kuwa katika utaratibu huu wa mchakato wa kuwapata wagombea,
chama hakitaingilia mamlaka waliyojiwekea na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) na kwa sasa tayari wale wote wanaohitaji kuchukua fomu za kuwa
wagombea, wanaweza kuchukua katika tarehe iliyopangwa.
Aliongeza
kuwa, fomu hizo zitaanza kuchukuliwa katika majimbo ambayo hayana
wawakilishi wao Bungeni ambapo majimbo yenye wawakilishi, fomu zitaanza
kutolewa hadi hapo Bunge litakapokuwa limevunjwa na mchakato mzima wa
utoaji fomu ukiwa tayari umehalalishwa.
Alitaja
viwango vya fomu vitakavyotumika katika kugombea ngazi ya urais hadi
udiwani kwa upande wa urais ni Sh.1,000,000, ubunge Sh.250,000 pamoja na
viti maalum. Udiwani wa kata ni Sh. 50,000 pamoja na udiwani wa viti
maalum.
Hivyo
fomu hiyo itarejeshwa kwenye jimbo au kata ambayo mgombea anagombea na
ndipo atapaswa kulipia gharama za fomu husika baada ya kuijaza na pia
fomu zitapatikana katika ‘website’ ya chama ambayo ni www.chadema.or.tz
Post a Comment