HUKU wakidaiwa kuogelea kwenye utajiri wa mabilioni
ya fedha, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibukia kwenye
Gazeti la Amani na kusema kuwa, amefunga ndoa ya kimyakimya na mpenzi
wake wa sasa, Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye ni nyota wa muziki wa kizazi
kipya, nchini Uganda na Afrika Kusini.
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari.
Diamond aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipofanya mahojiano
na waandishi wetu baada ya kumuuliza kama ana mpango wa kufunga ndoa na
Zari.
SIKIA MAHOJIANO HAYO
Amani: “Zari ameshakubebea ujauzito, ameshaandaa shoo ya nguvu ile ya Zari All White Party hapa kwenu Tanzania na ameonekana kukubalika na baadhi ya mashabiki wako. Je, una mpango gani wa kufunga naye ndoa sasa?
Diamond: “Khaa! Mbona kama ni ndoa na Zari nimeshafunga kimyakimya!”
Amani: “Si kweli bwana! Lini na wapi?”

Diamond: “Hapahapa Dar. Lakini siwezi kusema ni wapi kwani
tulishaamua iwe kimyakimya na imepita tayari, siku chahe kabla ya ile
shoo ya Mlimani City.”Amani: “Kama ni kweli kwa nini haikuwa na
mashamsham kama ndoa za mastaa wengine?”
KISA CHA KIMYAKIMYA
Diamond: “Unajua bi mkubwa (mama yake mzazi, Sanura Kasim) alikuwa anaumwa, kidogo ana nafuu kwa sasa. Ndiyo maana sikutaka mashamsham.”Amani: “Zari mwenyewe amekubaliana na uamuzi wa ndoa ya kimyakimya?”
Diamond: “Hakuwa na shida.”

KUHUSU DINI YA ZARI
Amani: “Amebadili dini? Maana ilisemekana alikuwa Muislam, akabadili kuwa Mkristo.”
Diamond: “Ilikuwa rahisi kurudi kwenye imani yake ya kwanza kwa hiyo ataendelea kuitwa Zarina.”

DIAMOND SASA
Rafiki wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini lakini wengi wanamjua, alipoulizwa kuhusu ndoa ya Diamond na Zari alisema:
“Jamani! Jamani! Jamani! Hivi kweli mnavyomjua Dangote (Diamond) nyie anaweza kufunga ndoa kwa siri au kimyakimya?”

...Wakipozi.
Amani: “Amesema kwa sababu mama yake bado hajakaa sawasawa kiafya?”
Rafiki: “Mbona kaenda kutumbuiza kwenye Zari All White Party, Mlimani City, si angekaa na mama yake nyumban? Hivi Dangote mnamjua, mnamsikia? Acheni kabisa.

“Dangote anapenda kiki! Kila siku anawaza kiki. Kwa hiyo kusema
amefunga ndoa na Zari sidhani kama ni kweli inaweza kuwa ni kiki. Tena
afadhali kama Zari asingekuwa na mimba, lakini ameshambebea ule mzigo
ndiyo kabisa maana Dangote yeye hana cha kupoteza. Lakini anyway, labda
kweli.”
NI SIKU CHACHE BAADA YA WEMA KUDAI AMEFUNGA NDOA
Hivi karibuni, mpenzi wa zamani wa Diamond aliye pia Miss Tanzania 2006 na staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu naye alitupia kwenye mtandao wa Instagram picha inayomwonesha amefunga ndoa kwa siri.

Baada ya picha hiyo kuwa gumzo, baadhi ya vyombo vya habari, hasa vya
kielektroniki vilimpigia simu Wema ili kumuuliza kama kweli amefunga
ndoa kwa siri kama inavyoenea kwenye mitandao, Wema alikiri.
Kwa ile sauti yake ndogo: “Yeah! Nimefunga kweli ndoa.”

Swali: “Sasa Wema wewe ni supastaa, kwa nini ufunge ndoa kwa siri mpaka wadau wako wasijue?”
Wema: “Mume wangu hapendi ijulikane. Hata mimi sipendi ijulikane.”

YALIYOMKUTA WEMA BAADA YA KUKIRI
Amani lilizungumza na mtu mwingine wa karibu na Wema ambapo alisema:
“Jamani Wema amejitakia matatizo, ndugu zake, dada yake na mama yake wamemjia juu. Kwanza walimuuliza kama ni kweli amefunga ndoa bila wao kujua, akasema hajafunga.

“Mama yake alimwambia alichokifanya cha kukiri kwenye redio ni nuksi
kubwa kwake na Watanzania hawatamwamini tena hata akisema ukweli.“Unajua
ndugu zake waliweka kikao. Walikubaliana kwamba, kama ndoa yake ilikuwa
kwenye filamu si mbaya lakini walilaani kile kitendo cha kuulizwa na
watangazaji wawili wa redio tena kwa muda tofauti akakiri. Pale ndipo
penye tatizo. Leo hii Wema atazungumza ukweli gani kwa watu
wakamuelewa?”
WEMA NA GAZETI LA AMANI
Wema alipotafutwa juzi na gazeti hili na kuulizwa kuhusu ndoa hiyo alikiri kuwa ilikuwa filamu ambayo itatoka hivi karibuni.

Post a Comment