Kocha Mzungu wa Simba, Goran Kopunovic amewaangalia mastaa wake wa kigeni na
kuona ni wawili tu wanaomfaa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kama
atasalia Msimbazi.
Kocha huyo amewataja wachezaji ambao angependa kubakishwa kikosini ni Emmanuel Okwi na Juuko Murshid, huku akimchambua Dan Sserunkuma kuwa si mshambuliaji anayeendana na mfumo wake kiufundishaji hivyo apigwe chini fasta.
Wengine aliopendekeza watemwe ni Simon Sserunkuma na beki kisiki, Joseph Owino huku akitoa mapendekezo ya kutaka mastaa watatu kutoka timu za Yanga, Azam na Mbeya City saini zao zisakwe haraka ili waingie kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kwa msimu ujao.
“Kati ya wachezaji watano wa kigeni waliopo Simba ni wawili tu, ndiyo wanaopaswa kubakizwa nao ni Okwi na Murshid, wengine waachwe kwani hawana msaada kwa klabu,” alisema Kopunovic ambaye ni raia wa Serbia.

Post a Comment