Hii ni ripoti kutoka Bungeni leo kuhusu mji unaoongoza kwa kesi za watuhumiwa wa ubakaji Tanzania (Audio)

Hii stori imetoka kwenye Kikao cha Bunge la Bajeti kilichoendelea leo May 18 2015 Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu lilikuwepo swali pia kuhoji juu ya Majiji yanayoongoza kwa kesi za ubakaji, jingine lilikuwa linahusu ishu ya nguo za wafungwa magerezani.
>>Ni Jiji gani linaongoza kwa uhalifu wa ubakaji na udhalilishaji na mikakati gani Serikali imeweka ili kupambana na uhalifu huu>> swali la kwanza la Mbunge Kidawa Hamid Salehe
Swali jingine la Mbunge Kidawa Salehe>>Suala la pili kuna taarifa kwamba baadhi ya Magereza yamekosa nguo za wafungwa.. wafungwa wanakuwa na nguo mbovu zinazoonesha miili yao, Serikali ina mkakati gani katika ili kuondokana na tatizo hili>>
Jibu la kwanza kutoka kwa Pereira Silima>> “Jiji ambalo linaongoza katika masuala ya unyanyasaji, wahalifu ambao wako magerezani la kwanza ni Tabora wahalifu wako 307 kwenye Gereza la Uyui, Tanga wako 110 na Arusha wako 80>>
Jibu la pili ni hili >> “Mahitaji halisi ya wafungwa ni angalau wapate jozi mbili kila mwaka, kuna tatizo kutokana na ufinyu wa Bajeti.. Kuna baadhi ya wafungwa wanavaa nguo zilizochanika ni sawa lakini hakuna mfungwa ambae anaenda uchi”>> Naibu Waziri Pereira Silima.
Iko sauti hapa pia, maswali na majibu yote utayasikia mtu wangu, bonyeza play

Post a Comment

Previous Post Next Post