Mambo vipi mpenzi msomaji wangu? Tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini uko poa.Leo tunaye mwanadada anayekwenda kwa jina la Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’.
Naye yuko hapa kujibu maswali 10 aliyobanwa na mwandishi wetu
Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’.
IMELDA MTEMA.
Ijumaa: Tulisikia unataka kuolewa, ukavishwa hadi pete ya uchumba, hili suala limeishia wapi?
Jack: Ndoa bado ipo, hapa kati nilisafiri ndo’ mambo yakasimama lakini nimerudi, muda wowote nitawaambia lini naolewa.
Ijumaa: Inadaiwa kuna wakati ulitishia kutaka kurudisha pete, nini kilitokea? Au ulipata mpenzi mwingine mwenye nazo?

Jack: Wala siyo kwamba nilipata mpenzi mwingine, kuna mambo
yalijitokeza ndiyo ikawa hivyo lakini sasa hivi hakuna shida, tuko sawa
kabisa.
Ijumaa: Najua una mtoto, hivi baba yake ni huyo mchumba wako wa sasa?
Jack: Siyo mtoto wake lakini amemkubali, anampenda na yuko tayari kumfanya awe kama wake.
Ijumaa: Ni misukosuko gani uliyokutana nayo katika safari yako ya umaarufu.
Jack: Dah! Ni mingi sana, wapo waliotaka kunitumia kama bigijii, wapo waliotangaza ndoa kumbe wanataka kunionja tu, nimepambana sana!
Ijumaa: Ulivyokwenda Thailand watu walikuwa wakisema umeenda kujiuza, unazungumziaje tuhuma hizo?
Jack: Unajua watu wengi wanapenda sana kuwazungumzia watu bila kuwajua na wanapenda sana vitu vya kuhisi bila kufikiria. Hayo ni maneno ya watu tu. Nilienda kwenye mambo yangu na wala siyo kujiuza jamani.
Ijumaa: Mastaa mnaandamwa sana na skendo za kuchukua waume za watu, unadhani ni kwa nini?
Jack: Ni kweli baadhi ya mastaa wa kike wana katabia hako lakini siyo wote. Mimi nadhani tunatakiwa kubadilika, wanaume wapo wengi tu kwa hiyo haina haja kuchukua ambaye tayari ana mtu wake.
Ijumaa: Kati ya mastaa wanaosifika kwa kuvaa nusu utupu, wewe umo. Ni kwa nini?
Jack: Kwa kweli ni nguo ambazo zinanifanya niwe huru, nikivaa ndefu labda naenda msibani.
Ijumaa: Wazazi wako wanajisikiaje wanapoona habari zako mbaya kwenye magazeti?
Jack: Najua hawapendi lakini mtoto wao nishakuwa staa kwa hiyo mambo kama hayo lazima wayazoee.
Ijumaa: Ni tukio gani katika maisha yako linakuumiza mpaka leo?
Jack: Yapo mengi lakini hili la kufiwa na mama yangu linauumiza moyo wangu hadi leo.
Ijumaa: Mastaa wanaonekana kutokuwa na damu ya kudumu kwenye ndoa, wewe unadhani utaimudu kweli?
Jack: Kutulia kwenye ndoa ni hulka ya mtu, nikiingia ujue siwezi kutoka na naweza kuwa mfano kwa wengine.

Post a Comment