Binadamu wamepoteza utu! Mwanamke mjamzito aliyefahamika kwa
jina la mama Janeth, mkazi wa Kimara-Suka jijini Dar anadaiwa kujifungua
kisha kukiweka kichanga kwenye begi na kukitupa shambani, kisa
kikielezwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi na mwanaume aliyempa ujauzito.
Mama anadaiwa kutupa kichanga hicho akijaribu kuangalia huku na kule kama kuna mtu anamuona alifahamika kwa jina la mama Janeth.
Mmoja wa mashuhuda akizungumza na gazeti hili, alisema kichanga hicho
kilikutwa na bibi anayejulikana kwa jina la mama Joyce katika shamba
lake lililopo eneo la Moa, Kimara-Suka baada ya kubanwa sana mama Janeth
alikiri kuwa ndiye mwenye kichanga hicho.
Kufuatia kuulizana ndipo mwenye shamba akakumbuka kuwa mama Janeth
alikuwa mjamzito na ilionekana alijifungua usiku, walipombana sana
alikubali kukitupa kichanga hicho.
Ijumaa Wikienda lilizungumza na mmoja wa mashuhuda ambaye
hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa mama huyo alipohojiwa alisema
mwanaume aliyempa ujauzito aliukataa ndipo akaamua kufanya kitendo
hicho.
Wananchi walifanikiwa kumtia mikononi mama Janeth na kumhoji ila
wakiwa wanajianda kuwaita polisi, mwanamke huyo alichoropoka kiaina na
kwenda kusikojulikana.
Baada ya polisi kufika eneo la tukio, mama Janeth alikuwa kishatoroka
na polisi wakalazimika kuwachukua baadhi ya majirani kwa ajili ya
mahojiano zaidi, huku mwili wa kichanga hicho ukipelekwa kuhifadhiwa
Hospitali ya Tumbi, Kibaha.
“Wanawake mnapaswa kuwa makini sana katika suala la uhusiano kwani
mnapokosea ndiyo chanzo cha kupata ujauzito na mwisho mnawatupa watoto
wenu, ” alishauri shuhuda huyo ambaye hakupenda jina lake liwe wazi
Post a Comment