Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, uvamizi wa
Saudi Arabia nchini Yemen umeyatia njia makundi ya kigaidi na kuyafanya
yajizadidi na kushadidisha mashambulizi yao nchini Somalia.
Ban amenukuliwa na shirika la habari la Associated Press akisema hayo
jana katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na
kuongeza kuwa, usalama wa Somalia na eneo hilo zima la Pembe na Afrika
na mashariki mwa bara hilo unatishiwa na uwepo wanamgambo wa ash Shabab
wenye mfungamano na al Qaida.
Matamshi hayo yamekuja katika hali ambayo tarehe 9 mwezi huu wa Mei,
makundi ya kitakfiri yalitangaza kuhusika na mauaji ya Mbunge wa
Puntland nchini Somalia, Said Hussein Nur, siku moja baada ya mbunge
huyo kupigwa risasi na kundi la watu waliokuwa wamejizatiti kwa silaha
wakati alipokuwa anatoka msikitini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehusisha matukio hayo na mashambulizi
ya Saudi Arabia nchini Yemen hususan kutokana na kuongezeka harakati za
kigaidi za makundi ya kitakfiri nchini Somalia tangu Saudia ilipoanzisha
mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen.
Nur ni mbunge wa pili wa Puntland kuuawa katika kipindi cha wiki chache
zilizopita. Mwezi uliopita pia, wanamgambo wa ash Shabab walimuua kwa
kumpifa risasi mbunge mwengine Aden Haji Hussein wakati alipokuwa
ziarani mjini Mogadishu.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
Post a Comment