Funguka! Mwanadada mwenye mvuto wa aina yake katika kiwanda
cha filamu Bongo, Ester Kiama ameibuka na kuwachana mastaa wa kike
wanaopenda kuiba waume za watu kwamba waache kwani si tabia nzuri.
Akizungumza Ester alifunguka kuwa mastaa
wanaochukua waume za watu, tabia zao siyo nzuri na kibaya zaidi
wakishawachukua wanajigamba ili watu wawaone wako juu mjini wakati
hawana lolote.
“Siyo kwamba sijawahi kuwa na mume wa mtu, nilishawahi lakini nimetokea kuwachukia sana kwani hawana faida zaidi ya kuwapotezea wasichana muda wao, nimejifunza mengi na sitarudia tena hivyo nawasihi wenzangu waache kuiba waume za watu kwani watarogwa tu,” alisema Ester.

Post a Comment