MWENGE WA UHURU WAZINDUA MAGARI YA UKUSANYAJI TAKA YA KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO LTD YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.6

Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Kisutu jijini Dar kwenye uzinduzi wa magari mapya ya kuzoa taka katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na na kampuni ya Green WastePro ltd. Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza jambo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika eneo la Kisutu jijini Dar kwa ajili ya ufunguzi wa Magari ya kisasa ya kuzoa taka.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2015 , Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto) akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
9
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mmoja wa viongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd aliwasisitiza wananchi kuendelea kutumia kampuni hiyo kwani usafi utaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kutoka kushoto), Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy(katikati) Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo( wa pili kutoka kulia) pamoja na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi katika eneo la Kisutu jijini Dar.
Mmoja wa viongozi wa mbio za mwenge akiwa ameshikiria Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuondoka mara baada ya kumaliza uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi mali ya kampuni ya Green Waste Pro Ltd inayofanya kazi za usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya M. Mngurumi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akiwa na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena wakiwa wanatoa maelezo juu ya uzoaji na usindikaji wa Taka zinazokusanywa katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala na jinsi ya watakavyoyatumia magari hayo yaliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Akizungumza wakati wakati wa tukio la uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi ya Kampuni iliyopewa zabuni kusafisha manispaa ya Ilala, Green Waste Pro Ltd Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kushirikiana vyema kwa kampuni Green Waste Pro Ltd ndiko kunako pelekea maendeleo na afya bora katika manispaa ya Ilala hivyo tuwaunge mkono wenzetu kwa kuwapa ushirikiano wa kuto tupa taka hovyo bali maeneo husika yaliyo wekwa kwaajili ya kuhifadhi taka hizo ili waweze kuzipitia kwa urahisi na kuzipeleka mahala panapo husika.

Post a Comment

Previous Post Next Post