NIKIACHIKA, NDOA TENA BASI- DAVINA

Staa wa filamu za Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ ameibuka na kusema kuwa kama itatokea ndoa yake ikawa ndiyo imevunjika kabisa hatarajii kuolewa tena, itakuwa ndiyo imetosha.
 
Staa wa filamu za Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.
Akizungumza hivi karibuni, Davina alisema anamshukuru Mungu kwa kubahatika kuonja tamu na chungu ya ndoa na sasa kama itatokea mumewe akaona waachane kabisa, hatakuwa na sababu ya kuhangaikia kuolewa tena.
“Yaani kama ndoa yangu itavunjika kwa kweli sihitaji ndoa ya aina yoyote tena katika maisha yangu, nitakachofanya ni kulea watoto wangu tu,” alisema Davina.

Post a Comment

Previous Post Next Post