MWANADADA
anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’
amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na vibaka ambao
walivunja gari lake na kuchukua vifaa mbalimbali na fedha dola elfu
moja za Marekani sawa na shilingi 1,900,000 za Kitanzania.
Mwanadada anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akielezea tukio hilo, Nisha alisema lilitokea usiku wa saa tisa
Jumapili iliyopita ambapo watu wapatao watano waliruka ukuta na kuingia
ndani na kuvunja gari lake aina ya Toyota Harrier na kuchukua vifaa
kibao zikiwemo taa na side mirror.
Mbali na kuchukua vifaa hivyo, pia wahalifu hao walichukua dola elfu moja alizokuwa amezisahau kwenye gari kabla ya majambazi hao kukimbia baada ya Nisha na mfanyakazi wake kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zao.
Mbali na kuchukua vifaa hivyo, pia wahalifu hao walichukua dola elfu moja alizokuwa amezisahau kwenye gari kabla ya majambazi hao kukimbia baada ya Nisha na mfanyakazi wake kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani zao.
“Dada ndiye alinishtua, aliniambia kuna watu wanavunja gari,
nilipochungulia dirishani nikawaona kama watano hivi, tukaanza kupiga
kelele za kuomba msaada, tukawaona wanakimbia na kupakia kwenye gari
lililokuwa nje wakatokomea,” alisema Nisha.
“Kweli nimeumia sana, inaonesha watu hawa walikuwa wananifuatilia
maana nilichelewa kurudi nyumbani na muda mfupi tu baada ya kurudi ndiyo
na wao waliingia, inauma sana,” alisema kwa majonzi msanii huyo.

Post a Comment