Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu akielezea umuhimu wa kufanya Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.
Kamishna wa Sensa
ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akitoa maelezo
mafupi kuhusu Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo
Dodoma.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Galawa akiwahutubia washiriki wa
Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.
Mmoja
wa washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012 akisoma Chati inayoonesha viashiria mbalimbali
vinavyotokana na Sensa hiyo. Semina hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Hazina ndogo Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Semina
ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012
wakifuatilia kwa makini semina hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa
Hazina ndogo Dodoma. ( PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
Na.Verinica Kazimoto. Dodoma
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo mkoani Dodoma imeendesha semina ya
usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2012 kwa viongozi na
watendaji wa ngazi mbalimbali wa mkoa huo kwa lengo la kuwajengea uelewa
viongozi hao waweze kuyatumia matokeo ya Sensa hiyo kupanga mipango ya
maendeleo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa Semina hiyo viongozi wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwemo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii Bw.Ephraim Kwesigabo na Kamishna wa Sensa ya Watu na
Makazi 2012 Hajjat Amina Mrisho Said wamesema viongozi na watendaji hao
wanayo kubwa ya kusimamia matumizi ya takwimu sahihi za Sensa hiyo.
Wamewasisitiza viongozi na watendaji hao kuzitumia takwimu za Sensa ya
Watu na Makazi 2012 katika kupanga mipango yao ya maendeleo ili waweze
kutatua changamoto balimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo
wanayoyasimamia.
Aidha, wametoa wito kwa viongozi hao kuzingatia matumizi ya takwimu
sahihi pindi wanapotenga fedha za bajeti kugharamia miradi mbalimbali ya
maendeleo katika sekta ya afya, maji, elimu, kilimo,mifugo na biashara
ili bajeti zao ziweze kukidhi mahitaji halisi ya idadi ya wananchi
wanaowahudumia.
Zoezi la Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2012 mbali na
mkoa wa Dodoma limeshafanyika katika mkoa wa Pwani na Morogoro.
Post a Comment