Mwaandishi mmoja mashuhuri kwa ripoti za upekuzi, Seymour Hersh, amekanusha madai ya utawala wa Rais Obama
kuhusiana na kuuawa kwa kinara mkuu wa kundi la wapiganaji la Al-Qaeda, Osama Bin Laden, nchini Pakistan miaka 8 iliyopita.
Akiandika
katika jarida la London Review of Books, Bwana Hersh, alikanusha madai
ya Washington kuwa, kutekwa na kisha kuuawa kwa kiongozi huyo wa AlQaeda
ilikuwa ni janja janja za shirika la kijasusi la Marekani CIA.
Hersh anasema ukweli ni kuwa walisaidiwa pakubwa na shirika la kijasusi la Pakistani.
Aidha kiongozi mkuu wa kijasusi wa Pakistan anasemekana kuongoza mikakati ya operesheni hiyo ya kisiri.
![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2014/12/15/141215110806_osama_bin_laden_black_flag_640x360_afp_nocredit.jpg)
Wakati ambapo Pakistan ilipojitenga na uvamizi huo na kuutaja kama ukiukaji wa uhuru na mipaka yake.
Marekani wala Pakistan hazijasema chochote hadi kufikia sasa.
Post a Comment